Wednesday, August 12, 2020

YANGA NGOMA INOGILE

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MWAMVITA MTANDA

WAKATI Yanga ikizidi kuwafukuzia watani wao wa jadi Simba katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Luc Eymael, amesema kuna kitu kinanukia Jangwani.

Yanga inayoshikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, inatarajia kushuka dimbani kesho kuvaana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, mchezo huo utaambatana na tukio la kuadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa klabu yao hivyo kutakuwa na ‘surprise’ kibao.

“Klabu yetu Jumanne (kesho) inaadhimisha miaka 85 tangu ianzishwe, sambamba na hilo, tutakuwa na mechi na Mbeya City Uwanja wa Taifa, ningependa kuwaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika tukio kubwa kama hili na la kihistoria, litaambatana na ‘surprise’ kibao na niwakumbushe wimbi la ushindi litaendelea,” alisema.

Wakati Mwakalebela akieleza hayo, Eymael amezidi kuwapa jeuri wapenzi wa klabu hiyo, akiwaambia angalau kwa sasa anaweza kuwaahidi kitu kwa jinsi anavyokiona kikosi chake.

Akizungumza na BINGWA jana, Eymael alisema awali hakuwa na jeuri ya kuahidi kitu kwa Wanayanga kutokana na jinsi alivyokuwa akikiona kikosi alichokikuta.

Alisema baada ya kukinoa kikosi hicho kwa muda mfupi, anaamini lolote linaweza kutokea msimu huu, kuanzia ubingwa wa Ligi Kuu Bara hadi Kombe la Shirikisho la Azam.

Alisema kikosi chake kimezidi kuimarika kiasi cha kuwawezesha kushinda mchezo wowote ule, huku akiahidi kuzidi kukiboresha kukifanya kuwa na makali zaidi.

“Sikuja Yanga kutembea, nimekuja kufanya kazi iliyo bora, niwaambie mashabiki wa Yanga huu ni mwaka wao wa kufurahi, uwezekano wa kuchukua ubingwa upo, cha msingi tushirikiane kuisapoti timu.

“Kila jambo lenye mafanikio, linahitaji umakini katika utendaji, ndio maana kila siku nawasisitiza wachezaji wangu kutimiza wajibu wao ambao umewaleta Yanga,” alisema. 

Mbelgji huyo alisema wapenzi wa Yanga watafurahi zaidi mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu Bara na kwamba mechi zao tatu zijazo, zitadhihirisha hilo.

Alisema kwa pengo lililopo kwa sasa baina yao na Simba, pointi saba, haoni sababu ya watu wa Yanga kutokuwa na matumaini na ubingwa wa Bara, akiamini lazima wapinzani wao hao watateleza, hasa baada ya kufungwa juzi na JKT Tanzania. 

Kwa upande mwingine, kocha huyo amemzungumzia straika wake, Muivory Coast, Yikpe Gislain, akiwataka mashabiki kutokuwa na hofu naye kwani tayari ameshagundua tatizo lake, akiahidi kulifanyia kazi.

“Yikpe ni mchezaji mzuri ambaye anatambua wajibu wake akiwa kazini, lakini upungufu wake upo kwenye balansi ya miguu, mashabiki wasiwe na hofu, kwa kushirikiana na kocha wangu wa viungo, tumeanza kumsadia, atakuwa fiti kabisa,” alisema Mbelgiji huyo.

Sambamba na hilo, Eymael amesema kuwa anahitaji mshambuliaji mwenye njaa ya mabao ili kukifanya kikosi chake kuwa tishio zaidi.

“Kwa kuwa muda wa usajili umepita, ninachofanya na msaidizi wangu Master (Charles Mkwasa) ni kuwapika hawa tulionao na kuwaelekeza jinsi ya kufunga mabao zaidi ambayo ndiyo kiu waliyonayo mashabiki kwa sasa, tunajua wanataka ushindi wa mabao mengi,” alisema.

Alisema iwapo ataendelea kuwapo Jangwani msimu ujao, dirisha la usajili wa kiangazi, atashusha vifaa vya nguvu, wakiwamo washambuliaji hatari zaidi ili kulitawala soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -