Saturday, November 28, 2020

YANGA NOMA, VIBOPA WATUA MWANZA KUZIKABIDHI KAZI MAALUMU MBAO, TOTO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR,

UKONGWE dawa asikuambie mtu kwani baada ya Yanga kushindwa kuwafunga Mtibwa Sugar na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wanajangwani hao wameamua kutumia uzoefu wao wa nje ya uwanja ili kuwazidi ujanja mahasimu wao Simba kuelekea mbio za ubingwa.

Unajua ikoje! Mabingwa hao watetezi wanajua kuwa Simba wanakabiliwa na michezo mitatu migumu Kanda ya Ziwa dhidi ya Mbao FC, Toto Africans pamoja na Kagera Sugar hivyo kuamua kuzikabidhi kazi maalumu ili kuwatibulia Wekundu wa Msimbazi hao.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa matajiri wa klabu hiyo wameshaandaa mpango wa kuzisapoti Mbao FC na Toto Africans ili kuiliza Simba watakapotia mguu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika msimamo wa ligi, Simba wana pointi 55 kileleni, wakiwazidi Yanga waliopo nafasi ya pili kwa pointi mbili baada ya timu zote hizo kushuka dimbani mara 24.

Rekodi zinaonyesha kuwa katika misimu kadhaa ya nyuma, Simba wamekuwa na wakati mgumu wanapokutana na Toto Africans Kirumba na sasa Yanga wameamua kuingiza miguu yote jijini Mwanza kuhakikisha wanaharibu kabisa mipango ya mahasimu wao hao huku pia wenyewe wakijipanga kushinda michezo yao yote iliyobakia.

Kigogo mmoja wa Yanga ambaye yupo katika Kamati ya Mashindano, ameliambia BINGWA kuwa hawawezi kuuachia ubingwa wao kirahisi hivyo kuweka mikakati ya kuzisapoti Mbao FC na Toto Africans za Mwanza kuhakikisha wanaifunga Simba watakapokutana nayo.

“Kwa sasa tunacheza kote kote, yaani ndani na nje ya uwanja, tunajua hawa ndugu zetu (Simba) wanakuwa na wakati mgumu sana wanapocheza na Toto Africans, sasa tunataka mambo yaharibike kabisa kwa kupoteza mchezo huo na ule dhidi ya Mbao.

“Hakuna ubishi kwamba tutatoa sapoti kubwa kwa hizi timu mbili za Mbao na Toto Africans kuhakikisha ‘Mnyama’ hachomoki na hilo linawezekana kabisa,” alisema kigogo huyo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mhandisi Paulo Malume, alisema japo Simba wamewaacha kwa pointi mbili, lakini watapigana kiume kuhakikisha wanamaliza michezo yote sita kwa ushindi.

“Bado tuna nafasi, wapinzani wetu wanaweza kupoteza na kutupa nafasi ya kupanda kileleni, kimsingi watu wote unaowajua wewe wapo karibu na timu isipokuwa hatutaki kuyatangaza mambo yetu, tumejipanga ndani na nje kuhakikisha ubingwa unabaki Jangwani,” alisema Malume.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema japo katika soka lolote linaweza kutokea, lakini uzoefu unaonyesha kuwa mechi za mikoani huwa ngumu kwa timu za Dar es Salaam hivyo hata Simba wanaweza kuteleza na kutoa mwanya kwao kutetea ubingwa wao.

Tayari imeelezwa kuwa mashabiki wa Yanga wa Dar es Salaam wataungana na wenzao wa Mwanza wakati Simba itakapokuwa huko ili kuongeza nguvu kuhakikisha Wekundu wa Msimbazi hao wanaangukia pua.

Yanga wenyewe wanataka kuona kwamba kama ikishindikana kabisa kuwazidi Simba kwa pointi basi zimalize ligi zikiwa sawa wakiamini kuwa watawazidi ujanja kwenye uwiano wa mabao ya kufunga.

Wanajangwani hao wanaamini kuwa kama Simba wakipata matokeo mabaya kwa Mbao na Toto Africans, hata wakija kupata matokeo mazuri dhidi ya Kagera Sugar, haitawasaidia chochote kwani watakuwa wameshapotea.

Mbali na mechi hizo tatu ambazo Simba watatoka, mechi nyingine tatu zilizobakia dhidi ya Stand United, Mwadui FC pamoja na African Lyon, Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa Uwanja wa Taifa ambapo pia mechi hizo zinatajwa kuwa si lele mama.

Simba inayonolewa na Joseph Omog, hesabu zake zimezidi kuwa ngumu, kwani ukuta uliopo Kanda ya Ziwa ndio unaotakiwa kuangushwa kama wanataka kufanikiwa katika azma yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Kitu kingine kinachowapa nafasi Yanga kutetea ubingwa wao msimu huu ni mechi tano ambazo watamalizia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Yanga wamebakisha mechi dhidi ya Azam FC, Mbao FC, Prisons na Mbeya City zote za Mbeya, Kagera Sugar na Toto Africans.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -