Monday, August 10, 2020

YANGA ROHO YA PAKA, WAPANIA KUANDIKA HISTORIA

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR,

KLABU ya Yanga inaondoka leo saa 12:00 jioni kiroho ngumu kuelekea nchini Algeria kuvaana na MC Alger katika mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, bila mshambuliaji wao Obrey Chirwa.

Kikosi hicho cha Yanga kitaondoka na wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Omari Hamadi mjini Algiers, baada ya ule wa kwanza Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na kiungo, Thaban Kamusoko katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam.

Hivyo, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kutinga hatua hiyo ya makundi.

Lakini Yanga wanahitaji kuwa ‘roho ya paka’ kwenye mchezo huo kwa kuwa watawakosa wachezaji wao saba akiwamo Chirwa kwa mujibu wa meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh.

Hafidh alisema wachezaji watakaoachwa mbali na Chirwa, ni mlinda mlango Ali Mustafa ‘Barthez’, Matheo Antony, Malimi Busungu, Yusuf Mhilo, Justine Zulu na Pato Ngonyani.

“Msafara wa wachezaji 20 na benchi la ufundi utaondoka kesho (leo jioni) na Shirika la Ndege la Emirates kupitia Dubai. Ila kuna wachezaji mbalimbali watabaki Dar es Saalam,” alisema Hafidh.

Meneja huyo aliwataja watakaondoka na timu leo jioni kuwa ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Beno Kakolanya, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Juma Abdul na  Andrew Vincent.

Wengine ni  Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geofrey Mwashiuya, Emanuel Martin, Amis Tambwe na Donald Ngoma.

Ingawa Hafidh hakutoa sababu ya wachezaji hao kuachwa, lakini BINGWA lilipata taarifa kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Salum Mkemi, akisema kwamba Chirwa hatasafiri kwa kuwa hati yake ya kusafiria imejaa.

“Hati ya Chirwa imejaa hivyo anatakiwa kurudi kwao Zambia kushughulikia, kwa maana hiyo haweza kuwahi mechi. Maana masuala ya hati ya kusafiria yana taratibu zake za kufuatilia,” alisema mjumbe huyo.

Naye Katibu Mkuu wa miamba hiyo ya Jangwani, Charles Boniface Mkwasa ambaye pia atakuwamo katika msafara huo, aliliambia BINGWA  kuwa maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika na wamejipanga vyema.

“Tunajua kutakuwa na mambo mengi ambayo si ya kiungwana kabla ya mchezo huo, lakini tumewaandaa nyota wetu kisaikolojia kwamba wasitoke mchezoni bali waelekeze akili zao kwenye mtanange huo,” alisema Mkwasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -