Tuesday, December 1, 2020

YANGA ROHO YA PAKA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

KLABU ya Yanga inaondoka leo saa 12:00 jioni kiroho ngumu kuelekea nchini Algeria kuvaana na MC Alger katika mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, bila mshambuliaji wao Obrey Chirwa.

Kikosi hicho cha Yanga kitaondoka na wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Omari Hamadi mjini Algiers, baada ya ule wa kwanza Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na kiungo, Thaban Kamusoko katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam.

Hivyo, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kutinga hatua hiyo ya makundi.

Lakini Yanga wanahitaji kuwa ‘roho ya paka’ kwenye mchezo huo kwa kuwa watawakosa wachezaji wao saba akiwamo Chirwa kwa mujibu wa meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh.

Hafidh alisema wachezaji watakaoachwa mbali na Chirwa, ni mlinda mlango Ali Mustafa ‘Barthez’, Matheo Antony, Malimi Busungu, Yusuf Mhilo, Justine Zulu na Pato Ngonyani.

“Msafara wa wachezaji 20 na benchi la ufundi utaondoka kesho (leo jioni) na Shirika la Ndege la Emirates kupitia Dubai. Ila kuna wachezaji mbalimbali watabaki Dar es Saalam,” alisema Hafidh.

Meneja huyo aliwataja watakaondoka na timu leo jioni kuwa ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Beno Kakolanya, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Juma Abdul na Andrew Vincent.

Wengine ni Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geofrey Mwashiuya, Emanuel Martin, Amis Tambwe na Donald Ngoma.

Ingawa Hafidh hakutoa sababu ya wachezaji hao kuachwa, lakini BINGWA lilipata taarifa kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Salum Mkemi, akisema kwamba Chirwa hatasafiri kwa kuwa hati yake ya kusafiria imejaa.

“Hati ya Chirwa imejaa hivyo anatakiwa kurudi kwao Zambia kushughulikia, kwa maana hiyo haweza kuwahi mechi. Maana masuala ya hati ya kusafiria yana taratibu zake za kufuatilia,” alisema mjumbe huyo.

Naye Katibu Mkuu wa miamba hiyo ya Jangwani, Charles Boniface Mkwasa ambaye pia atakuwamo katika msafara huo, aliliambia BINGWA kuwa maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika na wamejipanga vyema.

“Tunajua kutakuwa na mambo mengi ambayo si ya kiungwana kabla ya mchezo huo, lakini tumewaandaa nyota wetu kisaikolojia kwamba wasitoke mchezoni bali waelekeze akili zao kwenye mtanange huo,” alisema Mkwasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -