Thursday, October 29, 2020

YANGA SASA NI SHIIIDA JAMANI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA MARTIN MAZUGWA

KAMA ukibahatika kushuhudia mazoezi ya Yanga yanayofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana chini ya kocha Mzambia, George Lwandamina, lazima utakubali kuwa sasa timu hiyo ni shiiida sana.

Na hii inatokana na ukweli kuwa kocha huyo anaonekana kutokutaka masihara kwenye kazi wakati huu ambao anawaandaa wachezaji wake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa.

Lwandamina ambaye amepania kuhakikisha Yanga inakuwa tishio barani Afrika, ameamua kuwatolea uvivu na kuwapa adhabu za hapa na pale wachezaji wake ambao wanaonekana kushindwa kufanya yale ambayo anawaelekeza.

Wachezaji waliokiona cha mtema kuni kwa Lwandamina ni pamoja na mastraika, Donald Ngoma, Malimi Busungu na Obrey Chirwa ambao walipewa adhabu ya kupiga ‘pushapu’ baada ya kushindwa zoezi la kupiga pasi zinazofika kwa walengwa.

Haji Mwinyi naye alipewa adhabu ya kupiga pushapu tano  kwa kushindwa kufunga bao baada ya shuti alilopiga kupaa.Kabla ya kupigishwa pushapu, Mwinyi alipigiwa makofi na Lwandamina baada ya kuwapiga chenga kadhaa mabeki wa timu hiyo, lakini kaponzwa na shuti lake lililopaa.

Kwa upande wa Vincent Bossou, Busungu yeye alipewa adhabu ya kukimbia na mpira kuzunguka koni mara tatu, Chirwa akifanya hivyo mara tano kwa kosa la kupoteza pasi.

Lakini wakati wachezaji kadhaa wa Yanga wakionja joto ya jiwe kutokana na makosa ya kupiga pasi, kiungo mpya wa timu hiyo, Justin Zulu, alithibitisha kuwa ni ‘pass master’ kutokana na kumudu vyema zoezi la kupiga pasi ambapo katika dakika 30 alizokaa uwanjani wakati wa mazoezi, hakupoteza pasi hata moja.

Thaban Kamusoko na Hassan Ramadhani ‘Kessy’ ni wachezaji wengine walioonekana kulimudu zoezi hilo la kupiga pasi ambalo lilisimamiwa kwa ukaribu sana na Lwandamina na Noel  Mwandila.

Kelvin Yondani, Haruna Niyonzima na Beno Kakolanya walishindwa kufanya mazoezi na wenzao kutokana na kuwa majeruhi.

Inadaiwa kuwa sababu za mazoezi ya timu hiyo kuanza saa nane mchana ni sehemu ya harakati za Lwandamina kuhakikisha timu hiyo inaua ndege wawili kwa jiwe moja, yaani inafanya vizuri kwenye ligi kuu na katika michuano ya kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -