Saturday, October 31, 2020

Yanga SC kukodishwa sawa, lakini…

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

KLABU ya soka ya Yanga, imefungua ukurasa mpya baada ya kukodiwa na kampuni ya Yanga Yetu kwa muda wa miaka 10 kuanzia Septemba mwaka huu, ikiwa ni baada ya maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Agosti 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa mkodishaji, mpango huo umefikiwa kama sehemu ya kutumia rasilimali za klabu ya Yanga ili kuinufaisha kiuchumi, ikiwa ni baada ya kujiendesha kwa kutegemea hisani zawatu wachache.

Kwa ujumla, ukongwe wa Yanga katika soka la Tanzania, ikiwa imeanzishwa takribani miaka 80 iliyopita, haulingani hata kidogo na maendeleo yake kiuchumi, ikiwa imeshindwa hata kumiliki uwanja wake wenye kiwango cha kutosha kucheza si tu mechi za kimataifa bali hata zile za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Matokeo yake, hata linapokuja suala la kufanya mazoezi ya maandalizi ya msimu au mechi, klabu hiyo imekuwa ikitumia viwanja vya kukodi, huku klabu iliyoanzishwa miaka michache iliyopita, takribani miaka tisa, Azam FC, ikiwa inamiliki uwanja wa kisasa wenye kila kifaa kinachotakiwa kwa mchezaji au timu kujifunzia au kutunza kiwango chake.

Ikumbukwe hayo yote yanatokea huku Yanga ikitajwa kuwa klabu yenye mashabiki wengi zaidi hapa nchini na kwingineko, ambao ni zaidi ya mtaji wa kuiendesha iwapo itapata usimamizi wa kisasa utakaohusisha wataalamu wa mambo ya soka.

Na kikubwa ambacho kinaonekana mtaji zaidi ndani ya klabu hiyo kulingana na idadi ya wanachama takribani 12,000, huku mashabiki wakitajwa kuwa zaidi ya milioni 20, ni nembo ya klabu hiyo ambayo ndio hasa imeishawishi Kampuni ya Yanga Yetu kuikodisha klabu hiyo.

Kupitia ukodishaji huo uliofanywa na Yanga Yetu uliotiwa saini na Baraza la Wadhamini ya klabu hiyo, nembo imetajwa kuwa msingi wa ukodishwaji huo ambapo itatumika kwa muda huo wa miaka 10 kuiingizia kipato timu ili kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi zilizokuwa ikiikabili kwa miaka nenda miaka rudi.

Lakini pia, mpango huo umetajwa kulenga kuiwezesha Yanga kutoendelea kujiendesha kihasara katika kipindi cha muda huo (miaka 10) ya ukodishwaji kwa kuhakikisha inajipanga kiuwezo ili timu ya mmiliki na hakimiliki za jina lake na nembo zitakaporejeshwa baada ya kukodishwa, klabu hiyo itakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe na uwezo wa kifedha na hivyo kushindana kikamilifu katika shughuli za soka.

Kwa mujibu wa mkataba baina ya Yanga Yetu na Baraza la Wadhamini, mkodishwaji atailipia klabu hiyo deni la Shilingi bilioni 11,676 inayodaiwa na kwmaba mkodishwaji atailipa Sh milioni 100 kwa mwaka ambayo klabu itawekeza kiwango kisichopungua asilimia 90 ili kuimarisha mtandao wa matawi yake.

Pia, imeelezwa kuwa Yanga Yetu itailipa Yanga katika mwaka wa fedha wowote ule kukiwa kuna faida ya fedha taslim ya asilimia 25 ya fedha ambayo klabu hiyo itaitumia kujenga uwanja wake wa soka katika eneo walilopewa lililopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na hayo na mengineyo, mkataba huo unaonyesha kuwa mkodishwaji ataanza kuwekeza kwa vitega uchumi kuanzia siku ya 90 ya mkataba katika mafunzo na vifaa, ambavyo kutakuwepo uwanja wa mazoezi, huku Yanga Yetu ikiahidi kuhakikisha timu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Lakini baada ya kutangazwa kwa mkataba huo baina ya Yanga Yetu na Klabu ya Yanga, wapo walioupongeza, huku wengine wakiuponda.

Kwa wale wanaouponda mpango huo wanadai kuwa hautakuwa na manufaa yoyote kwa Yanga na wanachama wake zaidi ya kunufaisha watu wachache, huku wanaousapoti wakiamini huenda ukawa mkombozi wao.

Yote kwa yote, watu wa Yanga wanatakiwa kujiuliza mambo kadhaa wanapofikiria lolote juu ya ‘ndoa’ yao na Yanga Yetu.

Kwamba kwa takribani zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo, nembo yao imewasaidia vipi? Kwamba ni kiasi gani cha fedha wamevuna kupitia nembo yao hiyo zaidi ya kuwanufaisha wajanja wachache?

Kama hakuna, kwanini wasite au kujiuliza mara mbili juu ya suala zima la mpango wao wa kuikodisha nembo hiyo kwa Yanga Yetu? Au wapo tayari kuendelea kuombaomba huku wajanja wachache wakiitumia nembo hiyo kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuvuna mamilioni?

Ushauri. Nadhani kinachotakiwa kwa watu wa Yanga ni kukaa na kuona ni vipi mkataba huo utawanufaisha. Kwa mgano kumpa muda mkodishaji mathalani miaka mitano kuhakikisha klabu hiyo inakuwa na uwanja wake wa kiwango cha kimataifa kwa ajili ya mechi na mazoezi, lakini pia kukarabati jengo lao lililopo Mtaa wa Twiga na Jangwani na lile la Mtaa wa Mafia.

Ni wazi iwapo pande hizo mbili zitakubaliana hilo na mkodishaji kulitekeleza kwa dhati kabisa, tena ndani ya muda mfupi, klabu hiyo itakuwa imejikomoa kwa kiasi fulani kutoka katika umasikini unaoikabili, zaidi ikiwa ni kuhaha kusaka viwanja vya mazoezi.

Katika hilo, ni vema kukawa na makubaliano ya muda kwamba iwapo hayo, yaani ujenzi wa uwanja, vitega uchumi na mengineyo hayatafanyika ndani ya muda wa makubaliano, mkataba huo ubatilishwe.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -