Thursday, October 22, 2020

YANGA SC MWENDO MDUNDO

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

NA WINFRIDA MTOI


*Wachezaji waruhusiwa kujivinjari na wapenzi wao

*Waapa kuendeleza mauaji Ligi Kuu Bara

YANGA hawapoi, kwani baada ya kuwasili nchini wakitokea Rwanda walikocheza na Rayon Sports ya huko katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, hasira zao zote wameamua kuzielekeza Ligi Kuu Tanzania Bara, wakipania kushusha kipigo kwa kila timu watakayokutana nayo.

Katika michuano hiyo ya kimataifa, Yanga imeshika mkia Kundi D kwa kujikusanyia pointi nne, kutokana na mechi sita, huku ikizishuhudia USM Alger ya Algeria na Rayon zikitinga robo fainali kutoka kundi lao hilo, wakati Gor Mahia ya Kenya ikishika nafasi ya tatu na kuhitimisha safari yao.

Kwa kushika nafasi mbili za chini, Yanga na Gor Mahia (pointi 8), kila moja itaondoka na kitita cha Dola za Marekani 275,000 (zaidi ya shilingi milioni 600), huku vinara, USM Alger (pointi 11) na Rayon (pointi 9), wakizoa Dola za Marekani 350,000(zaidi ya Sh milioni 700), lakini pia wakiwa na nafasi ya kupata fedha zaidi jinsi timu itakavyofanya vizuri hatua za nusu fainali na fainali.

Katika mchezo wao huo wa juzi dhidi ya Rayon mjini Kigali, Rwanda, Yanga walifungwa bao 1-0, ushindi uliowawezesha wenyeji wao kusonga mbele.

Kikosi cha Yanga kimetua nchini jana na leo kinatarajia kuanza mazoezi rasmi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam, kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.

Hadi sasa Yanga wamecheza mechi moja ya ligi hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini.

Akizungumza na BINGWA kwa simu jana akiwa njiani kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya taifa ya nchini kwao huko, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema kwa sasa nguvu zao zote wanaelekeza katika ligi.

Zahera alisema yeye anaondoka, lakini programu yote amemwachia kocha wa viungo ambaye ndiye msaidizi wake, Noel Mwandila, huku akiwapa wachezaji wake mapumziko ya siku moja, yaani jana tu ili kwenda kujivinjari na wapenzi wao, kuanzia wazazi, watoto, wake au wachumba zao, ndugu, jamaa na marafiki.

“Nimewaambia wachezaji wakifika wapumzike, lakini kesho (leo) waanze mazoezi, nimempa kocha msaidizi programu ya siku 10, naamini muda huo utatosha kukiweka kikosi sawa kwa ligi.

“Tumeshatoka katika mashindano (ya kimataifa), kwa sasa tunaekeza nguvu zaidi Ligi Kuu, tunataka kufanya vizuri kwasababu lengo letu ni ubingwa, hakuna kingine tunachotafuta,” alisema Zahera.

Alisema kuwa, kiwango walichoonyesha wachezaji wake dhidi ya Rayon ni kizuri, kwani kiliwafanya wapinzani wao kupata bao kwa bahati.

“Wachezaji wangu walikuwa vizuri katika mchezo na Rayon, hivyo programu niliyompa kocha msaidizi, itaendelea kuwaimarisha na kuondoa makosa yaliyoonekana katika mechi zetu zilizopita,” alisema.

Kwa upande mwingine, Mkongomani huyo aliwatupia lawama waamuzi wa mchezo wao huo wa juzi kwa kuwabania, lakini pia akielezea jinsi mvua ilivyonyesha na kuufanya uwanja kujaa maji kuwatesa mno vijana wake.

Mchezo ujao wa Yanga wa Ligi Kuu Bara utakuwa dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, mjini Shinyanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -