Saturday, November 28, 2020

YANGA: SIMBA IMEKULA KWENU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

YANGA wameipiga mkwara Simba na kuwaambia ‘imekula kwenu’ kutokana na kuwa na uhakika wa kuwashushia kipigo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Februari 25 mwaka huu, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wamepiga mkwara huo baada ya kushtukia janja za mahasimu wao hao, ambao wanadaiwa kutuma makachero wao kuchunguza mazoezi waliyokuwa wakifanya kwenye Uwanja wa Taifa.

Baada ya kushtukia makachero hao, Yanga  inayonolewa na kocha George Lwandamina, iliamua kubadili uwanja wa mazoezi na kwenda Chuo cha Polisi uliopo Kurasini, ambako kuna ulinzi wa hali ya juu.

Makachero hao wa Simba bila kujua jana asubuhi waliibuka Uwanja wa Taifa na kuduwazwa kwa kuwakosa mahasimu wao, ambao walikuwa Chuo cha Polisi wakijifua kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ngaya de Mbe ya Comoro, utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa.

Yanga wanajua wakicheka na nyani watavuna mabua, hivyo kukwepa kuhujumiwa na watani wao hao wa jadi katika mchezo huo wa Februari 25, wamehamia kwenye uwanja huo wa Chuo cha Polisi wakipiga marufuku hadi mashabiki kuchungulia kwenye ukuta wa chuo hicho na wamekuwa wakiwakamata wote ambao wanachungulia wakikwepa hujuma hizo.

Pamoja na Yanga kuwa na mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao awali walishinda mabao 5-1 ugenini, lakini wamekuwa wakijifua zaidi na mchezo huo wa Ligi Kuu kwa kuwa wana uhakika wa kuwatoa Ngaya na kusonga mbele.

Kikosi hicho cha Lwandamina kilifika Uwanja wa Taifa jana asubuhi kufanya mazoezi, lakini baada ya majadiliano marefu waliamua kuondoka na kwenda kwenye uwanja huo wa Chuo cha Polisi na kuwaacha mashabiki wao waliofika kuangalia mazoezi wakishangaa wasijue cha kufanya na wengine kudhani kwamba wasingefanya mazoezi kabisa.

Lakini kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh, aliyezungumza na BINGWA, walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo wa Taifa, lakini walipokumbuka Simba watakuwa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya African Lyon waliamua kuhama na kusema ndio msingi wa mabadiliko hayo.

“Jana (juzi) nilikwambia tutafanya mazoezi hapa Taifa, lakini asubuhi (jana) yalitokea mabadiliko ambayo yalitupasa kuhama kwa sababu tuligundua Simba wana mechi jioni kwenye uwanja mkubwa tukaona tufanye Polisi,” alisema.

Lakini chanzo cha ndani kinadaiwa kwamba uongozi wa Yanga uligundua makachero wa Simba wametumwa kuchunguza watani wao hao wa jadi, hivyo wakaamua kuhama ili kuficha mbinu zao.

Simba watashuka dimbani kwenye mchezo huo wa Februari 25, mwaka huu wakiwa wanaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 51, huku Yanga wakishika nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 49, lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -