Sunday, November 1, 2020

Yanga: Simba walinzi wetu

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

YANGA wana dharau hatari. Unajua ni kwanini? Wakati Simba wakiendelea kujitanua kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku wakijiapiza kwamba hawatashuka hata kwa dawa, watani wao hao wa jadi, wameibuka na kudai kuwa Wekundu wa Msimbazi hao wanawalindia nafasi hiyo kwa muda.

Simba wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 13 kutokana na michezo yao mitano waliyocheza mpaka sasa, huku Yanga wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 10, lakini wakiwa wamecheza michezo minne tu.

Katika michezo hiyo mitano ambayo Simba wamecheza, wamefunga mabao nane na kufungwa mawili, huku Yanga nao wakiwa wamecheka na nyavu mara nane, lakini wakionekana kuwa na safu kali ya ulinzi, kwani hawajaruhusu bao lolote.

Kauli ya Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm kwamba wana uhakika wa kutetea ubingwa wao msimu huu, inalandana na ile ambayo inatolewa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kwamba Simba wapo kileleni kama walinzi na ‘mwenye nyumba’ (Yanga) muda wowote atahitaji kukaa kwenye nafasi yake.

Akizungumza na BINGWA jana, Pluijm alisema ana imani kwamba kikosi chake kitaweza kutetea ubingwa wake na malengo aliyonayo ni kuhakikisha hawapotezi mchezo wowote, japo hata wapinzani wao katika ligi wamejipanga vizuri.

“Nikizungumzia kwanza mchezo wetu dhidi ya Stand United, utakuwa mgumu, kwani kila timu imejipanga vizuri sana, ila nikuhakikishie kwamba kila kitu kiko vizuri na namshukuru Mungu sina majeruhi mpaka muda huu, isipokuwa Godfrey Mwashiuya.

“Kuhusu ubingwa, niseme kwamba hatuogopi timu yoyote, tunajua malengo yetu ni nini, katika soka unatakiwa kuangalia kila kilichopo mbele yako na hicho ndicho tunachokifanya, nawaamini vijana wangu,” alisema.

Kauli hiyo inaendana na tambo za mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakitamba kuwa hakuna chochote kitakachowazuia kutwaa ubingwa na kwamba Simba wanawashikia tu nafasi yao ya kukaa kileleni kwa muda.

Rafael Mnandi, ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga, aliliambia BINGWA akisema: “Pale kileleni tumewaachia Simba watulindie kwa muda, wao ni kama walinzi wetu kuzuia timu nyingine, hasa Azam FC wasifike pale, ila muda wowote tutarudi kwenye nafasi yetu.”

Naye Shaaban Kipingu alisema: “Ni rahisi kuwashusha Simba wanapokuwa kileleni kuliko timu kama Azam, Mtibwa au Mbeya City… Simba ni wasindikizaji tu kama ilivyokuwa msimu uliopita, walikaa kileleni na wenyewe tulipokalia kiti chetu, hakuna aliyeweza kutuzuia hadi tulipotwaa ubingwa.”

Kauli hizo zimeungwa mkono na mashabiki wengi wa Yanga, ambao wamesema timu hizo zitakapokutana Oktoba Mosi, mwaka huu, ndipo Wanajangwani hao watakaporudi rasmi kwenye nafasi yao ya kukaa kileleni, kwani wana uhakika wa kuwafunga Wekundu wa Msimbazi hao.

Msimu uliopita, Simba iliuanza vizuri kabla ya kuanza kuyumba na kujikuta wakibaki kuzisindikiza Yanga na Azam, zilizomaliza katika nafasi mbili za juu, huku ubingwa ukitua Jangwani.

Katika mechi baina ya watani hao wa jadi katika soka la Tanzania, Yanga walifanikiwa kuwatambia wapinzani wao hao kwa kushinda mechi zote mbili kwa mabao 2-0.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -