Saturday, November 28, 2020

YANGA VS AZAM ILIKUWA MECHI YA MBINU ZAIDI, MAELEKEZO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

Azam wameshindwa kuendeleza ubabe wao wa kuinyima ushindi Yanga baada ya juzi kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Tangu mwaka 2014, Yanga ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Azam katika kipindi hicho, timu hizo zilikutana mara sita kabla ya jana, zikitoka sare katika michezo mitano na Azam wakashinda mchezo mmoja.

Bao pekee lilofungwa na straika Obrey Chirwa lilitosha kupeleka vigelegele Jangwani ambapo kwa ushindi huo, Yanga imerejesha matumaini ya kutetea ubingwa wao baada ya kurejea kileleni.

Tukiangalia mchezo huo kwa jinsi ulivyochezwa ndani ya dakika 90, kuna mengi ya kuzungumzwa kiufundi kwa timu zote.

Ni mchezo uliojaa mbinu na maelezo

Ilikuwa tofauti kwa timu zote mbili Azam waliingia uwanjani wakiwa na mbinu ya kumiliki mchezo, lakini pia wachezaji walitakiwa kuzingatia maelekezo ya benchi la ufundi.

Azam waliingia uwanjani wakiwa na mbinu ya kumiliki mchezo, lakini pia wachezaji wake walitakiwa kuzingatia sana maelekezo ya benchi la ufundi.

Mromania Aristica Cioba alijaza viungo wengi ili kufanya timu yake itengeneze nafasi za mabao, uwapo wa Salum Abubakari ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Daniel Amoah na Himid Mao, ilionyesha wazi kwamba kocha huyo alikuwa na mbinu ya kuwakata kabisa Yanga na viungo wawili wa kulinda ukuta na wawili wa kupandisha mashambulizi kwa kumlisha Yahaya Mohammed.

Kwa upande wa Yanga ni kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao, waliingia wakiwa na mbinu zao za kuwaadhibu Azam walijaza viungo pia, Justin Zulu, Said Juma Makapu walifanya kazi ya kulinda ukuta Deus Kaseke na Haruna Niyonzima nao wakafanya kazi ya kulisha safu ya ushambuliaji, mbinu za kocha George Lwandamina zikagongana na Cioba.

Lwandamina alifahamu Azam wataingia na staili gani ndio maana akaamua kutumia mipira mirefu kwa wachezaji wake wa safu ya mbele na alijua wazi kwamba vita ya kati ingekuwa kubwa sana ndiyo maana akaamua kupanga kikosi namna ile.

Hawa walitisha

Obrey Chirwa kwenye mchezo huo alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuweza kuifungia timu yake bao pekee la ushindi lililoirudisha timu hiyo kileleni.

Ana kasi na pia ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Mara nyingi alikaa na mpira mguuni kuhakikisha anawavuta mabeki wa Azam ili kutoa nafasi kwa wenzake kufunga, lakini mabeki wa Azam walikuwa na nidhamu ya hali ya juu sana na hawakuruhusu hilo.

Chirwa, mashabiki wa Yanga walimuita ‘kiboko ya mabishoo’ Kweli! Alidhihirisha hilo alihakikisha anapambana kwa dakika zote ili timu yake ipate bao.

Saidi Makupu tangu kuja kwa Lwandamina amekuwa akipata nafasi mara kwa mara ya kucheza. Ana uwezo wa kulinda mabeki wake kama alivyofanya kwenye baadhi ya michezo aliyocheza.

Niyonzima, fundi huyu wa mpira alijitahidi kufanya kila lililowezekana kufikisha mipira kwa Chirwa, lakini umakini wa mabeki wa Azam  ulizuia pasi zake nyingi.

Safu ya ulinzi Yanga

Katika mchezo huo, safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa na kazi moja tu, kuwasoma washambuliaji wa Azam na kugundua wanapita katika njia gani na kujuua namna ya kuwazuia.

Kiuhalisia wa mchezo, Vincent Bossou alikuwa ni nyota katika safu ya ulinzi ya Yanga, akitumia vizuri uzoefu wake kwa kuwasoma washambuliaji wa Azam.

Utulivu wa Bossou, akili ya haraka iliweza kumsaidia beki huyo aliyekuwa akifanya kazi mubashara kabisa na mkongwe Nadir Haroub ‘Canavaro’.

Mipango ya ushambuliaji

Pacha wa Chirwa kwenye safu ya ushambuliaji Yanga alikuwa ni Simon Msuva ambaye alitumia nguvu zake kuukokota mipira na kuelekea lango la wapinzani.

Kiufupi Chirwa alitengeneza nafasi za kutosha katika mchezo huo. Ilidhaniwa Deus Kaseka angekuwa msaidizi wake  mkubwa katika ‘move’ zote alizokuwa akifanya, lakini hakuna mtu ambaye alionesha utayari wa kufanya hivyo na kushuhudia nafasi za muhimu zikipotea.

Lakini nafasi moja aliyoipata Chirwa iliweza kupeleka kilio Azam ambapo uzembe wa mabeki ulitosha kupeleka shamra shamra Jangwani.

Uzoefu uliwasaidia Yanga

Lazima tukumbuke Yanga ina watu wanaojua namna ya kucheza mechi na si kuchezea mpira, lazima ujue kuna kuchezea mpira na kucheza mechi kwa ajili ya timu kupata matokeo.

Uzoefu waliokuwa nao Yanga na ‘plan’ waliyokuja nayo haikuwa ni ya kushambulia sana, kwa walioutazama mchezo kwa umakini watakuwa ni mashahidi.

Baada ya kufunga bao hilo, Yanga wakarudi nyuma na kuwaacha washambuliaji wa Azam peke yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -