Monday, November 30, 2020

YANGA VS SIMBA NA SURA TATU ZA BONIFACE MKWASSA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA JESSCA NANGAWE

PAMOJA na ukongwe wa timu za Simba na Yanga, mchezo baina ya timu hizi za watani wa jadi umekuwa ukileta hamasa kubwa kwa mashabiki wa timu hizi kila zinapokutana.

Jumamosi hii Simba na Yanga zitashuka dimbani tena kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuonyeshana ubabe ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya mzunguko wa kwanza kutoka sare ya 1-1.

Moja ya mambo yanayovutia kwenye pambano hili ni ukongwe wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa ‘Master’ ambaye kwa sasa anaweka historia mpya katika pambano la watani wa jadi. Amelicheza pambano hilo akiwa mchezaji wa Yanga, amelicheza akiwa kocha na sasa analicheza akiwa Katibu Mkuu wa Yanga.

Mkwasa ambaye anaifahamu klabu ya Yanga tangu miaka ya 70 akiwa kama mchezaji, anasema kazi yake sasa ni kuona klabu hiyo inafika mbali katika michezo ya kitaifa na kimataifa lakini mambo yote yanayohusu ufundi analiachia benchi la ufundi.

Anasema pamoja na nafasi yake ya katibu ndani ya Yanga, bado ana jukumu kubwa la kulishauri benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na kocha raia wa Zambia, George Lwandamina ambaye anasaidiana na kocha mzawa Juma Mwambusi.

Akiwa mchezaji wa Yanga

Mkwassa anasema alianza kuitumikia klabu hiyo mwaka 1978 akiwa mchezaji na ndio kipindi ambacho klabu hiyo ilianza kujengeka upya.

“Mwaka 1975 Yanga iliingia katika mgogoro mkubwa na kupelekea kusambaratika kuanzia viongozi hadi wachezaji, nakumbuka sisi ndio tulianza kuijenga upya Yanga kuanzia miaka ya 76 – 79 hadi ikasimama vizuri,” anasema.

Katika kipindi changu cha uchezaji nimecheza mechi kadhaa za Yanga na Simba, zipo tulizoshinda, kutoka sare na kufungwa, najua ugumu wa mechi hii nikiwa kama mchezaji, najua maandalizi yake kama mchezaji najua presha ambaye anakuwa nayo mchezaji linapofika pambano hili.

Akiwa kocha wa Yanga

Mkwassa anasema kazi ya kuifundisha Yanga aliianza siku nyingi na alikuwa akiipenda kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa.

Alianza rasmi kuifundisha Yanga mwaka 1992 akisaidiana na marehemu Syllersaidy Mziray ambapo walifundisha kwa mafanikio makubwa.

“Nilianza kuifundisha Yanga nikiwa na kocha marehemu kwa sasa Mziray,  ambapo mechi yetu ya kwanza kupambana na watani zetu Simba ilikuwa mwaka 1992 na tulifanikiwa kuwafunga mabao 2-0,” anasema.

Anasema baada ya kuifundisha Yanga kwa misimu kadhaa alihama na kwenda kwenye majukumu mengine ikiwamo kuifundisha Al Shoula kabla ya kukabidhiwa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’.

“Ninajua ugumu wa mechi ya watani, nafahamu vyema presha ambayo kocha anakuwa nayo na ni ‘automatic’ inakuja, kwangu haikusumbua sana lakini nikwambie tu nalijua pambano la Yanga na Simba vizuri zaidi kwa sababu nimelicheza uwanjani na nikiwa nje ya uwanja,” anasema.

 

Akiwa katibu wa Yanga

Uongozi wa Yanga baada ya kuona uwajibikaji wa Boniface Mkwassa ndani ya klabu hiyo, waliamua kumteua kama Katibu Mkuu wa Yanga akitokea kwenye majukumu ya kocha mkuu wa Taifa Stars ambapo mpaka sasa anashikilia nafasi hiyo.

“Kwa sasa mimi ni Katibu Mkuu wa Yanga, kazi yangu kubwa ni kuiwezesha  timu katika mambo mbalimbali ya kiutawala na hata ya uwanjani, lengo letu ni kuona Yanga inafika mbali katika michuano mbalimbali,” anasema.

Anasema unapozungumzia ushindani wa Simba na Yanga, matokeo huwa ni baada ya dakika 90 kutokana na historia ya timu hizo.

“Unajua hizi timu kwa sasa zimegeuka kuwa na upinzani mkali zaidi kutokana na teknolojia inavyokwenda, kwanza miaka ya sasa wachezaji wa kigeni wamekuwa wakiongeza ushindani mkubwa na pia tangu zamani matokeo  ya timu hizi huwa ni ngumu kutabiri hivyo ni vyema kusubiri mpaka mpira umalizike,” anasema Mkwasa.

“Lakini kwa uzoefu wangu wa mechi hizo tangu nikiwa mchezaji, kocha na hadi sasa sioni kama tutashindwa, ningependa kujenga rekodi yangu vizuri kwa kuwa na mafanikio mbele ya Simba, nikiwa mchezaji, kocha na sasa kiongozi,” anasema Mkwassa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -