Friday, October 30, 2020

YANGA WAJIZATITI KILA KONA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

*Wakimbilia Zenji kupata baraka za wazee wao

*Lengo ni kuhakikisha wanauendeleza moto wao Ligi Kuu Bara

KATIKA kuonyesha jinsi walivyopania kuwaumbua Simba waliokuwa wakitambia usajili wao wa wachezaji mahiri uliogharimu shilingi bilioni mbili, Yanga wamejizatiti kila kona kuhakikisha wanawashangaza watani wao hao wa jadi kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wakiwa wameutwaa msimu uliopita baada ya kuusotea kwa misimu mitano bila mafanikio.

Kwa kipindi chote hicho, Yanga ndio waliokuwa wakijinafasi na taji hilo, wakilibeba mara nne, huku Azam wakilitwaa mara moja, msimu wa 2013/14.

Hadi sasa, Yanga hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya sita waliyocheza, wakishinda mitano na kupata suluhu moja dhidi ya Simba, hivyo kujikusanyia pointi 16.

Kwa upande wao, Simba wameshapoteza pointi saba katika ligi hiyo yenye timu 20, wakishinda mechi nne, sare mbili na kupoteza moja dhidi ya Mbao FC, hivyo kujizolea pointi 14.

Pamoja na usajili wao kubezwa na mashabiki wa Simba, lakini kasi yao Ligi Kuu Bara imekuwa ya aina yake hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa tofauti na ilivyokuwa ikitarajiwa mara baada ya dirisha la usajili kufungwa.

Katika kuonyesha jinsi Yanga walivyopania kufanya kweli msimu huu, klabu hiyo imejipanga kila idara kuanzia benchi la ufundi hadi nje ya uwanja.

Mathalani, pamoja na kucheza bila Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera, Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ngumu ya Mbao iliyoichapa Simba.

Katika mchezo huo, kikosi hicho cha Jangwani kilikuwa chini ya kocha wa viungo, Noel Mwandila ambaye aliwaongoza vema vijana wake kupata ushindi huo mnono uliozidi kuwapandisha mzuka mashabiki wao wakiamini msimu huu ni wao.

Wakifahamu wanacheza bila kocha wao mkuu, wachezaji wa Yanga walipambana hasa na kuwabana Mbao waliokuwa moto wa kuotea mbali, huku mshambuliaji wao, Ibrahim Ajib, akipiga bonge la bao linalopewa nafasi ya kuwa bao bora la msimu.

Lakini kwa nje ya uwanja, mambo si haba kwani klabu hiyo imeendelea na mikakati yake ya kujiimarisha na safari hii kikimbilia Zanzibar kunoa zaidi makali ya kikosi chao kuelekea mechi zijazo za ligi hiyo.

Mchezo ujao wa Yanga utakuwa ni dhidi ya Alliance ya Mwanza utakaopigwa Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Kutokana na umuhimu wa mchezo huo na mingine ijayo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda kujifua zaidi Zanzibar ambapo Jumamosi kitashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na Malindi, Uwanja wa Amaan.

Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh, alisema maandalizi yote kuelekea katika safari hiyo yamekamilika na kikosi hicho kitaondoka kesho mchana kwenda visiwani humo.

“Tunaendelea na mazoezi kama kawaida, lakini tunategemea kwenda kucheza mchezo mmoja wa kirafiki Zanzibar dhidi ya Malindi na mara baada ya kucheza mchezo huo, timu itarejea Dar es Salaam kuendelea na mazoezi yake,” alisema Saleh.

Alisema kikiwa Visiwani humo, kikosi hicho kitapata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za utalii kisha kupata baraka za wazee wenye mapenzi na timu hiyo kama sehemu ya kuwaongezea hamasa wachezaji wao waweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wake, Mwandila alisema ameridhishwa na namna vijana wao wanavyopokea mafunzo yao, akiamini kadiri muda utakavyozidi kwenda timu hiyo itazidi kuwa tishio.

“Mazoezi yanaendelea vizuri, programu niliyokabidhiwa na kocha Zahera inaendelea kufanya kazi, lakini cha kufurahisha ni jinsi wachezaji walivyo na morali ya juu, jambo linalonipa moyo wa kufanya vizuri zaidi mbeleni,” alisema Mwandila.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -