Friday, October 30, 2020

YANGA WAKESHA KUMJADILI NGASSA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

>>Hatimaye wafikia mwafaka baada ya kupiga kura

NA HUSSEIN OMAR

HATIMAYE Mrisho Ngassa anaweza kurejea katika kikosi cha Yanga, baada ya viongozi wa klabu hiyo kujifungia usiku kumjadili, ikiwa ni saa chache tangu alipoonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo baina ya Wanajangwani hao na timu yake ya Ndanda FC.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara, Ngassa alicheza vizuri mno na kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Yanga.

Pamoja na Yanga kushinda mabao 2-1, Ngassa aliiongoza vema timu yake kulitisha lango la timu yake hiyo ya zamani katika misukosuko, ikiwamo kuchangia kwa kiasi kikubwa bao lao la kufutia machozi.

Winga huyo aliyewahi kutamba pia katika vikosi vya Azam, Simba na timu ya Taifa, Taifa Stars, dakika ya 46 alichomoka kwa kasi ya ajabu na kuiwahi pasi iliyopigwa ndani ya 18 kabla ya kuubetua mpira na kumpita kipa wa Yanga, Youthe Rostand na kumkuta Nasoro Kapama aliyeusindikiza nyavuni.

Baada ya mchezo huo, viongozi wa Yanga walikutana katika hoteli waliyofikia mjini Mtwara na kumjadili Ngassa kuona kama ana nafasi kwenye kikosi chao au la.

Habari kutoka kwa mmoja wa viongozi waliokuwapo katika kikao hicho, zinasema kuwa walikuwa wakitofautiana juu ya mchezaji huyo mwenye mapenzi ya dhati na Yanga na kuamua kupiga kura.

“Lilipokuja suala la kura, wengi walikubali Ngassa arejeshwe Yanga, wachache tu wakimpinga kwa madai ya umri kumtupa mkono. Uzuri ni kwamba hata kocha (Lwandamina) anamkubali, sasa kilichobaki ni kusubiri kipindi cha usajili wa nyongeza wa michuano ya kimataifa kuona kama tunaweza kumchukua,” alisema kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani kwa kuwa kikao hicho kilikuwa ni cha siri.

Alisema suala hilo la usajili wa Ngassa limeachwa mikononi mwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika.

Kuonyesha jinsi alivyo na mapenzi na Yanga, baada ya mchezo wao huo wa juzi, Ngassa alifika katika kambi ya timu yake hiyo ya zamani akiwa na nyota mwingine wa zamani wa Jangwani, Salum Telela, ili kuwajulia hali wachezaji na viongozi.

BINGWA lilimtafuta Ngassa kuzungumzia kama yupo tayari kurejea Yanga na iwapo amefuatwa na kiongozi yeyote wa klabu hiyo, lakini simu yake haikuwa ikipatikana kila alipopigiwa.

Lakini BINGWA lina taarifa kuwa Ngassa alitakiwa Yanga tangu msimu uliopita, lakini ilidaiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga, hakuwa akimtaka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -