Sunday, November 29, 2020

Yanga walikosea lakini Pluijm amekosea zaidi

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HASSAN DAUDI

WIKI kadhaa zilizopita habari iliyokuwa ikizungumzwa sana kwenye medani ya michezo hapa nchini ni ile iliyohusu ujio wa kocha mpya katika klabu ya Yanga.

Macho na masikio ya mashabiki wengi wa kandanda yalielekezwa kwa kocha raia wa Zambia, George Lwandamina, ambaye kwa mujibu wa taarifa alikuwa anakuja kuchukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm.

Ni ngumu kuukosoa uamuzi huo wa Yanga kwani kilichowavutia kwa Lwandamina ni mafanikio yake akiwa na klabu ya Zesco United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia.

Lwandamina ameiwezesha Zesco kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo haikushangaza kuwaona Yanga wakitolewa udenda na huduma ya kocha huyo.

Kwa miaka kadhaa Yanga imekuwa ikijaribu bila mafanikio kujenga utawala wake kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika kwa ngazi ya klabu. Ni wazi Yanga walikuwa wakimhitaji Lwandamina kwa namna yoyote ile.

Lakini sasa harakati hizo za kumchukua Lwandamina hazikufuata weledi na hilo lilipelekea Pluijm kutangaza kujiuzulu wadhifa wake wa kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo.

Ndiyo, kitendo kilichofanywa na Yanga cha kuanza na kukamilisha taratibu za ujio wa Lwandamina bila kumpa taarifa yoyote Pluijm, hakikuwa cha kiuungwana.

Ingawa ilidaiwa Pluijm angekuwa mkurugenzi wa ufundi klabuni hapo, kwanini kocha huyo aliishia kuzisikia taarifa hizo kupitia vyombo vya habari?

Bila shaka Pluijm alitakiwa kuwa wa kwanza kujua mabadiliko hayo ya benchi la ufundi hata kabla ya taarifa hizo kuvifikia vyombo vya habari.

Kama ni kweli Yanga walitaka kumpa ukurugenzi Pluijm, kulikuwa na kosa gani kuupa kipaumbele uzoefu alionao kocha huyo katika kumsaka mtu sahihi wa kuchukua nafasi yake?

Walichokifanya Yanga ni kama vile walikuwa na ugomvi na Pluijm na hawakutaka ajue kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, baada ya kutangaza kujiuzulu pamoja na kuwaaga wachezaji wake, Pluijm alirejea kwenye benchi la ufundi la Yanga kutokana na ushawishi mkubwa wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Kwa upande mwingine, kuna taarifa zinazodai kuwa Yanga wamejishtukia, hivyo wamemtuma Nchemba kumrejesha kocha wao huyo.

Lakini pia, taarifa nyingine ambazo nazo hazijathibitishwa zimesema Yanga wameshindwana na Lwandamina.

Imeelezwa kuwa kocha huyo ametoa masharti mazito ikiwemo kuwa na jopo kubwa la wasaidizi wake wa benchi la ufundi.

Kwa upande wa Nchemba, ni ngumu kumkosoa waziri huyo kwa kile alichokifanya kumrudisha Pluijm Jangwani kwani ana haki ya kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba ni mwanachama wa Yanga.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa Pluijm alikurupuka na badala yake alitakiwa kufikiria mara mbili kabla ya kukubali kurudi kwenye benchi la ufundi la Yanga.

Pluijm alitakiwa kujiuliza, kwani aliikosea nini Yanga mpaka ifikie uamuzi wa kumfuata Lwandamina kimya kimya bila kumshirikisha?

Mbali na mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, aliiongoza Yanga kuliweka kabatini Kombe la FA.

Baada ya mateso ya muda mrefu kwenye michuano ya kimataifa, Pluijm ndiye aliyeiwezesha Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Ni wazi ulikuwa ni mwanzo mzuri kwa Yanga katika mashindano ya nje ya nchi na hakuna anayejua nini kingefuata katika mashindano ya mwakani!

Kwa upande mwingine, kabla ya kuamua kurudi Yanga, Pluijm alifikiria kuwa wale waliomuona hafai kuendelea kukinoa kikosi hicho wakisema uwezo wake umefikia kikomo, ndiyo atakaofanya nao kazi na si Nchemba?

Haijalishi kama Yanga ndiyo waliomtuma Nchemba au waziri huyo alifanya kwa mapenzi yake, ila Pluijm alipaswa kusimamia kile alichokiamini ambacho ni sahihi kwa asilimia 100.

Aliamini kuwa Yanga hawamhitaji na ni wazi ilikuwa hivyo na kama walitaka kumpa ukurugenzi ilikuwa ni ‘aibu’ yao kwa kocha huyo kutokana na mafanikio aliyokipa kikosi chao.

Kukimbilia kurudi Yanga kunaweza kumfanya kuwa mtumwa wa wale waliokuwa wakipigania aondoke na huenda sasa akafanya kazi katika mazingira magumu zaidi.

Pia, huenda hata heshima yake kwenye soka la Bongo ikashuka, wengi wamemuona kama kocha asiye na uhakika wa kazi nje ya Yanga.

Haimaanishi kuwa Pluijm hakutakiwa kurudi Yanga, lakini alitakiwa kuonyesha umuhimu wake kwa kuwasumbua walau wapate somo kuwa walikuwa wakipomteza mtu muhimu.

Kama alivyosema wakati anatangaza kujiuzulu kwa kile alichoifanyia Yanga kwa kipindi chote alichokaa Jangwani, Pluijm ana ‘CV’ za kumfanya apate kazi katika klabu yoyote ndani na nje ya nchi.

Kuthibitisha hilo, kulikuwa na tarifa zilizodai kuwa wakali wa Chamazi, Azam FC, walikuwa karibu kufuatilia kilichokuwa kikiendelea kati ya Yanga na Pluijm.

Ilielezwa kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikuwa ukivutiwa na mpango wa kumsainisha kocha huyo kama Yanga wangeamua kumpotezea.

Pluijm hakutakiwa kuwa mwepesi kiasi kile katika kubadili uamuzi wake, alipaswa kuwatingisha kidogo Yanga na hilo lingethibitisha ubora wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -