Sunday, January 17, 2021

YANGA WALIVAMIA KAMBI YA SIMBA 1981

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HENRY PAUL

UNAPOZUNGUMZIA matukio yaliyowahi kuwasikitisha Simba yaliyofanywa na watani wao wa jadi Yanga, kamwe huwezi kuacha kulitaja tukio la kuvamiwa kambi yao Shirika la Elimu Kibaha mwaka 1981, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kupambana katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu).

Kabla ya mechi hiyo, Yanga waliwachanganya kisaikolojia Simba kwa kuvamia kambi yao waliyokuwa wakitumia miaka mitano Shirika la Elimu Kibaha kwa kuweka kambi ya takribani mwezi mmoja chini ya kocha mkuu, Ray Gama, ambaye hivi sasa ni marehemu.

Yanga kabla ya kucheza mechi hiyo walikuwa wateja wa Simba kwa takribani miaka mitano kuanzia mwaka 1976 ikiwemo mwaka 1977 walipofungwa idadi kubwa ya mabao 6-0.

Yanga kutokana na kuwa wateja wa Simba kwa muda huo wote wa miaka mitano, hivyo mwaka huo wa 1981 waliamua kuwawahi Simba kwa kuweka kambi pale Kibaha ambako kulizoeleka miaka yote kuwa ni kambi ya wapinzani wao Simba.

Pia kwa upande mwingine viongozi hao wa Yanga wakiwa hapo Kibaha kujiandaa na kucheza na watani wao Simba waliamua mchezo huo usimamiwe na viongozi kutoka mikoani ambao walikuwa na mapenzi makubwa na timu hiyo akiwemo mzee Felician (baba yake Fumo Felician, mchezaji wa zamani wa Yanga) kutoka Mwanza, Adam Bailu kutoka Arusha na mmoja tu kutoka hapa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni mzee Mzimba (marehemu).

Uvamizi huo wa Yanga katika kambi ya Simba kwa kiasi kikubwa ulizaa matunda, kwani katika mchezo wao uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (sasa Uhuru), Jumamosi Septemba 5, 1981 walishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Juma Mkambi ‘General’ ambaye hivi sasa ni marehemu.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Yanga wakipeleka mashambulizi makali ya mfululizo langoni mwa wapinzani wao, huku mabeki wa Simba wakionekana kuwa na kazi moja tu ya kujitahidi kudhibiti mashambulizi hayo.

Katika dakika ya 35, Yanga walifanya shambulio moja la nguvu langoni mwa timu ya Simba na beki wao wa kushoto, Ahmed Amasha, aliyekuwa amepanda mbele kupiga krosi langoni mwa lango la Simba na mpira huo kutolewa nje na beki wa kulia, Daudi Salum na kuwa kona.

Kona hiyo ilichongwa na Amasha, nahodha Juma Mkambi, aliruka juu na kuwazidi mabeki wawili, Mohamed Bakari ‘Tall’, Aloo Mwitu na kupiga kichwa mpira uliotinga wavuni huku kipa Omari Mahadhi akijitahidi kudaka bila ya mafanikio.

Simba baada ya kufungwa bao hilo walijitahidi kushambulia kwa lengo la kutaka kusawazisha, lakini muda wa mapumziko nao ukawa umewadia. Hivyo mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika walikwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi ile ile kama walivyoanza nayo katika kipindi cha kwanza huku mabeki wa Simba wakionekana kuwa na kazi moja tu ya kujitahidi kudhibiti mashambulizi hayo.

Pamoja na Yanga kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Simba, lakini hakufanikiwa kupata bao lingine. Hivyo hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Yanga walitoka uwanjani vifua mbele kwa kuwafunga Simba bao 1-0 na kufuta uteja wa miaka mitano.

Hivyo kwa maneno mengine unaweza kusema kuwa uvamizi huo wa Yanga katika kambi ya Simba kwa kiasi kikubwa uliwasaidia, kwani waliwachang’anya kisaikolojia wapinzani wao na hatimaye kuwafunga bao hilo pekee 1-0.

Kikosi cha Yanga kiliwakilishwa na kipa; Hamisi Kinye, Athumani Juma ‘Chama’, Ahmed Amasha, Issihaka Hassan ‘Chukwu’, Allan Shomari, Juma Mkambi ‘General’ (marehemu), Shabani Katwila ‘Suzuki’/Charles Kilinda, Charles Boniface ‘Master’, Rashid Hanzuruni (marehemu), Omari Hussein ‘Keegan’, Saleh Hija/Ahmad Omari.

Kikosi cha Simba kiliwakilishwa na kipa Omari Mahadhi (marehemu), Kiwhelo Mussa (marehemu), Mohamed Kajole (marehemu), Aloo Mwitu, Mohamed Bakari ‘Tall’, Issihaka Mwitu, Rahim Lumelezi, Nico Njohole, Jumanne Masmenti (marehemu), Adam Sabu (marehemu) na George Kulagwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -