Friday, October 30, 2020

YANGA WALIVYOTWAA UBINGWA WA BARA MGONGONI KWA COASTAL UNION

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HENRY PAUL

ILIKUWA ni shangwe ya mashabiki wa klabu ya Yanga ilitawala kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union.

Matokeo hayo yaliiwezesha timu ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa sasa Ligi Kuu katika mchezo uliochezwa Septemba 3, mwaka 1989 kwenye uwanja huo.

Baada ya matokeo hayo mashabiki wa Yanga walifanya shangwe walipokuwa wanatoka kwenye uwanja huo wakiwa vifua mbele  kwa ushindi huo.

 Licha ya shangwe hiyo, pia ushindi huo iliipa Yanga tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Klabu Bingwa ya Soka Afrika.

Bao hilo muhimu la Yanga lilipatikana dakika ya 61 baada ya kiungo mkabaji wa Coastal Union, Idrissa Ngulungu, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Mussa Lyaunga kutoka Rukwa, kuamuru kupigwa penalti . Penalti hiyo ilifungwa kwa ustadi na beki wa kulia Fred Felix ‘Majeshi’.

Ushindi wa Yanga ulionekana dhairi toka walipopata bao dakika ya 35 lililofungwa na mshambuliaji Mwessa Kiwhelo na kukataliwa na mwamuzi kwa vile mfungaji alikuwa ameotea.

Baada ya kukoswa kufungwa bao hilo, Coastal Union walikuja juu na kuanza kufanya mashambulizi ya haraka haraka langoni kwa timu ya Yanga, hali iliyowalazimisha mabeki wa Yanga na kipa wao Sahau Kambi kufanya kazi ya ziada kuokoa.

Pamoja na mashambulizi hayo makali ya Coastal Union kufanywa na washambuliaji Hussein Mwakuruzo, Kassa Mussa, Razak Yusuf ‘Carecca na Mohamed Kampira, lakini kipindi cha kwanza hawakufanikiwa kupata bao.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika timu zilikwenda mapumziko matokeo yakiwa ni sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku Yanga wakilishambulia lango la Coastal Union mfululizo. Mashambulizi hayo yalikuwa yakifanywa na JustIne Mtekere, Mwessa Kiwhelo, John Alex na Athumani China.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -