Friday, October 30, 2020

Yanga wamrejesha Mkwasa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR,

KUFUATIA sare ya kufungana  bao 1-1  na Simba katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuliboresha benchi la ufundi kwa kumrejesha kocha wao msaidizi, Charles  Mkwasa.

Mkwasa, ambaye  kwa  sasa ni kocha mkuu wa Taifa Stars, anapigiwa chapuo na mashabiki wa klabu hiyo ili aweze kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la Wanajangwani hao.

Kocha huyo aliyefanya kazi kwa mafanikio makubwa akiwa na Pluijm kabla ya kwenda kuifundisha Stars iliyokuwa inakabiliwa na michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia na ile ya Afrika (AFCON), mashabiki hao wameanza kuona umuhimu wake,  baada ya timu yao kufanya vibaya baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Wakizungumza na BINGWA katika nyakati tofauti, mashabiki walisema kuna haja ya kumrejesha Mkwasa kutokana na kiwango hafifu kilichoonyeshwa na wachezaji wao kwa mechi za ligi hiyo.

Mmoja wa shabiki wa klabu hiyo kutoka tawi la Tandale kwa Mtogole, Juma Hamisi,  alisema hakuna ubishi Mkwasa anatakiwa kurejea Yanga kutokana na Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi kuonekana kuelemewa na kushindwa kumpa ushauri.

“Timu haina mpango B pale inapoonekana kuzidiwa kimchezo. Ni kocha Pluijm ameshindwa kupata mshauri pale mambo yanapokwenda vibaya, hivyo basi bora Mkwasa arudi, yule ni mkali anajua kumshauri kocha,” alisema Juma.

Juma alisema mechi dhidi ya Simba,  timu yao ilizidiwa kipindi cha pili na Pluijm alionekana na kushindwa kuwa na mpango mbadala.

“Si kocha tu, hata wachezaji wapo majipu, tunaomba uongozi wetu umrejeshe Mkwasa, bado tunamhitaji katika kipindi hiki ambacho mwakani tunacheza michuano ya kimataifa”.

Kwa upande wake, Abass Said alisema hajaridhishwa na kiwango cha wachezaji wa timu hiyo, kwani kocha mwenye uwezo wa kumshauri Pluijm kama Mkwasa anahitajika.

BINGWA lilimtafuta Mkwasa ili kuweza kuzungumzia kilio cha mashabiki wa timu hiyo, ambapo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia lolote.

Mkwasa alisema anawashukuru mashabiki hao kutokana na kutambua mchango wake, lakini kwa sasa bado ni kocha wa Stars.

“Mimi kama unavyojua sina lolote la kuwaambia zaidi ya kutambua kuwa nina mkataba wa kuifundisha timu ya Taifa, lakini nashukuru mashabiki wa Yanga kwa kutambua mchango wangu na kuithamini kazi yangu,” alisema Mkwasa.

Alisema amesikia kilio cha mashabiki hao na kusisitiza kila binadamu ana haki ya kuwasilisha hisia zake pale mambo yanapomfika shingoni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -