Wednesday, November 25, 2020

YANGA WANATELEZA TU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

yanga 2NA MWANDISHI WETU, MORONI

WANATELEZA TU!  Hili ndilo neno sahihi kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ambao jana walipata ushindi mnono wa mabao 5-1 ugenini mbele ya wenyeji wao Ngaya de Mbe ya Comoro.

Mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade de Bomel mjini Moroni, ulishuhudia Yanga ikianza kwa kasi na kuutawala sana mchezo huo huku winga wake, Simon Msuva, akipoteza nafasi kadhaa za kuifungia timu hiyo katika dakika za mwanzoni.

Ushindi huo umeiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo, kwani inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele ambapo huenda itakutana na Zanaco ya Zambia au APR ya nchini Rwanda ambao katika mechi yao ya kwanza mwishoni mwa wiki, zilitoka suluhu jijini Kigali, Rwanda.

Yanga na Ngaya watavaana tena katika mchezo wa marudiano Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Katika mchezo wa jana, Yanga walianza kuandika bao katika dakika ya 38 likifungwa na Justine Zulu, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Obrey Chirwa akiwa nje ya eneo la hatari.

Ngaya walikuja juu na kuishambulia Yanga na dakika ya 41, mshambuliaji wao, Hamis Toihir, aliwatoka mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali ambalo hata hivyo lilidakwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Msuva aliwania tena vitini mashabiki wa Yanga waliohudhuria mchezo huo katika dakika ya 45 kwa kufunga bao la pili akipokea pande safi la Thaaban Kamusoko na kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Ngaya wakijaribu kutafuta bao la kwanza bila mafanikio.

Lakini dakika ya 57, Yanga waliongeza bao la tatu kupitia kwa Chirwa ambaye aliitumia vema pasi iliyotoka kwa Kamusoko.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la Ngaya na walipata bao la nne dakika ya 64 likifungwa na Amissi Tambwe, akiwa ndani ya 18 baada ya  kupokea pasi kutoka kwa Juma Abdul.

Dakika ya 66 Ngaya walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji wao, Said Anphane, akiwa ndani ya 18.

Kamusoko alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 73 kwa Yanga kufunga bao la tano, baada ya kupasiana vema na Juma Mahadhi. Kikosi cha Yanga baada ya mechi hiyo kilifanya mazoezi mepesi kwenye uwanja huo na kisha kwenda uwanja wa ndege ambapo ilitarajiwa kurejea usiku wa jana jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania na nahodha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta anayecheza katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, ameipongeza Yanga kwa kupata ushindi huo na kuitaka Yanga kupata ushindi wa mabao 7-0 kwenye mchezo wa marudiano.

 

Samatta alitoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa akaunti ya Twitter ambao amekuwa mara kwa mara akizungumza masuala mbalimbali yanayotokea kwenye soka la Tanzania na katika mambo mengine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -