Monday, November 30, 2020

YANGA WANG’OA MWAMUZI MWINGINE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI,

MWAMUZI aliyechezesha mechi ya Ligi Kuu Soka ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga na Ruvu Shooting, Ahmada Simba, ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa ligi hiyo.

Simba anakuwa mwamuzi wa pili katika msimu huu wa ligi kuu kuondolewa katika mechi zinazoihusisha Yanga, mwingine ni Martin Saanya, aliyechezesha mechi ya mzunguko wa kwanza baina ya Yanga na Simba.

Saanya aliondolewa kwa madai alishindwa kumudu mchezo uliochezwa Oktaba mosi mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania maarufu Kamati ya Saa 72, haikuridhishwa na uchezeshaji wa  mwamuzi Simba, hivyo kumwondoa kwenye orodha ya waamuzi.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, ilieleza kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya utetezi wa mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa, ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi ya njano.

Tukio hilo lilitokea katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Machi mosi mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alisema kadi ya njano ya kwanza aliyopewa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 iliifuta kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8), haikupaswa kutolewa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.

Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi nyekundu, baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.

Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza, kunaifanya kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wake ni kadi hiyo iliyosababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angepaswa kukosa michezo miwili.

Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa ambayo Chirwa alionywa kwa utovu wa nidhamu.

Pia Yanga imepigwa faini ya Sh 500,000  kwa kitendo cha kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mchezo wao dhidi ya Simba uliochezwa Februari 25, mwaka huu.

Kitendo hicho ni kwenda kinyume na kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi, hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Yanga imepigwa faini hiyo.

Previous articleSIMBA WAIPIGA BAO YANGA
Next articlePIGA HAOO
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -