Monday, November 23, 2020

YANGA WAPEWA BONGE LA SOMO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA NEEMA STEPHEN, TSJ

WANACHAMA, wapenzi na mashabiki wa Yanga, wametakiwa kusahau yaliyopita kutokana na kipigo cha mikwaju ya penalti 4-2 kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba na badala yake kuganga yajayo.

Jumanne ya wiki hii, Yanga ilitolewa na Simba katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan kutokana na kipigo hicho, hivyo kutishia mparaganyiko ndani ya Wana-Jangwani hao.

Kwa kulifahamu hilo, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Athuman Kihamia, amewaambia wanachama na mashabiki wao kuwa wanachotakiwa kwa sasa ni kushikamana na kuona ni vipi wanajipanga kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Yanga ni timu kubwa hivyo kupoteza mchezo kwa penalti dhidi ya Simba, kusituumize vichwa na badala yake tujipange upya ili tuweze kufanya kweli katika mechi zetu zijazo, lakini kubwa zaidi ikiwa ni kulipa kisasi kwa kuwapiga mabao Simba tutakapokutana nao mwezi ujao katika mchezo wa Ligi Kuu Bara,” alisema Kihamia ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Kihamia pia aliwataka wachezaji kuhakikisha wanatimiza majukumu yao, wakifahamu mashabiki wao wamekuwa wakitumia muda na fedha zao kuisapoti timu hiyo kokote inakokwenda kutokana na mahaba waliyo nayo kwa ‘chama’ lao hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -