Sunday, October 25, 2020

YANGA WAPEWA HABARI NJEMA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

Kocha Mkuu wa Yanga,  Mwinyi Zahera, ametamba kuwa timu yake itaendelea kufunga mabao ya ‘kideo’ kila watakapokutana na wapinzani wao katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na ubora wa vijana wake.

Zahera alitoa kauli hiyo juzi, baada ya nyota wake Ibrahimu Ajib na Mrisho Ngassa kila mmoja kufunga bao maridadi katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata Yanga dhidi ya Alliance ya Mwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waliopeleka furaha kwa Wanajangwani hao ni Heritier Makambo, ambaye ni raia wa DR Congo pamoja  na winga machachari, Ngassa na Ajib.

Akizungumza na BINGWA juzi, Zahera, alisema hashangai kuona Yanga wakifunga mabao ya ‘kideoni’ kwani wanachokifanya mazoezini wachezaji wake ndicho hicho wanakifanyia kazi katika mechi.

“Bado huu ni mwanzo tu, magoli mengi sana yenye ubora yataendelea kufungwa na vijana wangu kwani wamekuwa wakijituma sana mazoezini, kinachotakiwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kuwapa morali wachezaji wao,” alisema Zahera.

Hii si mara ya kwanza kwa nyota wa Yanga kufunga mabao ya ‘kideoni’ kwani Ajib alijithibitisha kama mmoja wa wachezaji tishio hapa nchini, akiwa na kipaji cha kipekee baada ya kufunga bao ‘bab kubwa’ lililoihakikishia Yanga ushindi siku iliyocheza na Mbao FC.

Akiwa nje kidogo ya 18, Ajib aliuona mpira uliookolewa na mmoja wa mabeki wa Mbao ukimfuata eneo alilokuwapo na kuupiga kwa mtindo wa ‘tik tak’, uliompa umaarufu mkali wa Ghana, Anthony Yeboah na mpira kujaa nyavuni.

Kabla ya kujaa nyavuni, mpira huo uligonga mwamba wa juu na kuipatia Yanga bao la pili.

Saa chache baada ya bao hilo, kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, aliliambia BINGWA kuwa atampa nafasi Ajib katika mchezo wa kikosi chake hicho dhidi ya Lesotho wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), zitakazopigwa mwakani nchini Cameroon.

Amunike alisema japo hakwenda Uwanja wa Taifa, lakini aliushuhudia mchezo huo kupitia runinga na kuvutiwa mno na kiwango cha Ajib, zaidi likiwa ni bao lake hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -