Wednesday, November 25, 2020

YANGA WASIWAANGUSHE WATANZANIA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

YANGA ni wawakilishi pekee wa Tanzania Bara waliobakia kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Timu hiyo imebakia kwenye michuano hiyo, baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Kwenye michuano hiyo, Yanga ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Wazambia hao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini waliangukia katika kapu la Kombe la Shirikisho, baada ya kutoka sare ya tasa katika mchezo wa marudiano uliochezwa Lusaka.

Yanga inaendelea kushiriki michuano hiyo, ambapo kesho wanatarajia kucheza na MC Alger ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo tunaona ni muhimu kwa Yanga kushinda kwa idadi ya mabao mengi ili waweze kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kusonga mbele.

Tunaamini kwamba, Yanga ina uwezo wa kuandika historia mpya kwa kuiondoa timu hiyo ya Ukanda wa Kaskazini.

Tunajua kwamba, MC Alger watakuwa wanatafuta bao la ugenini ili waweze kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kusonga mbele wanaporudiana nchini kwao.

Kutokana na hilo, Yanga wanatakiwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani kupata ushindi mkubwa ambao utawaweka wapinzani katika hali ngumu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Tunasema kwamba, Yanga hawatakiwi kurudia makosa kama waliyofanya kwa Zanaco kwa kuruhusu bao nyumbani lililowapa fainali wapinzani wao kusonga mbele Ligi ya Mabingwa.

Litakuwa ni kosa kubwa likitokea kwa mara nyingine kuruhusu bao kwa MC Alger, kwani linaweza kuwaweka katika mazingira magumu zaidi watakapokuwa ugenini.

Kwa upande wetu, tunaamini kuwa benchi la ufundi la Yanga litakuwa limeweka mikakati ya kuhakikisha wanashinda baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojikeza kwenye mechi za awali za kimataifa.

Tunasema kwamba Yanga wanatakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, lakini wakicheza kwa kujituma zaidi kwa dakika zote 90 ili kuhakikisha wanashinda na kuwapa raha mashabiki wake.

Tunamaliza kwa kusema Yanga wasiwaangushe Watanzania kwa kufungwa na MC Alger nyumbani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -