Wednesday, October 28, 2020

YANGA WATAMBA SIMBA WAMEWATANDIKIA JAMVI, SASA HAWANA BREKI HADI UBINGWA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WAANDISHI WETU,

KATIKA wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Shariff Thabit ‘Darasa’ wa Maisha na Muziki, kuna mashairi yanayosema: “Unataka kukimbia na hauna breki” na “Vitu vingine havitakagi ujuaji, ukajikuta unawatandikia watu jamvi.”

Unajua nini? Saa chache baada ya Yanga kuifunga Mwadui mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi na kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo, wameanza nyodo wakiyatua mashairi hayo ya Darasa.

Wanajangwani hao wametamba kuwa kamwe hawatakubali kung’olewa kileleni, hivyo watani wao wa jadi, Simba waliokuwa wakiongoza ligi hiyo kwa muda mrefu, imekula kwao.

Walipoulizwa jeuri hiyo wameipata wapi wakati wametofautiana na Simba pointi moja tu, Yanga walitamba kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki.

Yanga wamefika mbali zaidi kwa kudai kuwa japo Simba walikaa kileleni kwa muda mrefu, hilo haliwapi shida wao kwani watani wao hao ni kama ‘wamewatandikia jamvi’ katika nafasi hiyo na kilichobaki kwao ni kujinafasi hadi mwisho wa ligi na hatimaye kulibakisha kombe Jangwani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Mhandisi Paul Malume, aliliambia BINGWA jana kuwa walichokuwa wakikitaka wao ni kukaa kwenye kiti cha uongozi na wamefurahi kufanikiwa katika hilo.

“Siku zote Simba huwa hawatuumizi vichwa, wamekuwa na kiherehere cha kukimbilia kileleni wakati uwezo wa kukaa huko hawana… Kama huna breki usipende kukimbiakimbia, wenyewe tumerudi katika nafasi yetu wamekwisha,” alitamba kigogo huyo wa Jangwani.

Kwa upande wake, kiungo wa kimataifa wa Yanga, Mzimbabwe Thaban Kamusoko, alisema: “Tumefurahishwa na kitendo cha kurudi kuongoza ligi, hivyo tuna imani tutaendelea kuongoza hadi mwisho wa msimu na kutwaa ubingwa.”

Kwa msimu wa tatu mfululizo, kila pale Yanga ilipokalia kiti cha uongozi wa ligi katika mzunguko wa pili, haijawahi kushuka hadi ilipotangazwa kuwa mabingwa.

Katika mchezo huo wa juzi, Mzimbabwe Obrey Chirwa ndiye aliyepeleka furaha Jangwani baada ya kuifungia timu yake mabao yote mawili dakika za 69 na 82, ikiwa ni baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

Ushindi huo umeiwezesha Yanga kufikisha pointi 46 na kuwazidi Simba kwa pointi moja.

Kwa takribani miezi minne, Yanga ilikuwa ikisota kuitafuta nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi, huku watani wao hao wa jadi wakiwakebehi kwa majina kede kede, likiwamo ‘Wazee wa Kifurushi’.

Kitendo cha Yanga kukalia usukani wa ligi, kinaonekana kuwa pigo kubwa kwa Simba ambao tayari walishaanza tambo za kutwaa ubingwa, baada ya kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi nane wiki tatu zilizopita.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Yanga wanapokuwa kileleni ni vigumu kuwashusha kama ilivyojitokeza msimu uliopita wa 2015/2016.

Katika msimu huo, hadi raundi ya 20 kama ilivyo sasa, Simba walikuwa wanaongoza ligi, lakini ilipofikia raundi ya 24, Yanga waliibuka na kukalia usukani hadi pale walipotwaa ubingwa.

Yanga msimu huu wanaonekana kuwa na faida zaidi ya mabao, hali inayozidi kuwapa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao iwapo hawatateleza, huku Simba wakizinduka na kurejea katika kasi yao.

Stori hii imeandikwa na HUSSEIN OMARI, ZAINAB IDDY NA WINFRIDA MTOI

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -