Wednesday, October 28, 2020

YANGA WATEGA, SIMBA WATEGUA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

SIMBA wajanja sana aisee asikuambie mtu kwani mitego yote waliyotegewa na wapinzani wao wa jadi, Yanga, wameitegua kwa asilimia 90 na hatimaye kurudi kwenye mstari ambapo iwe iwavyo, ndani ya wiki hii wanaweza wakarudi kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wekundu wa Msimbazi hao ambao walikuwa wakiongoza ligi kwa muda mrefu, wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 48 nyuma ya Yanga wenye pointi 49 na kwamba iwapo watashinda mchezo wao wa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wanaweza kuwashusha wapinzani wao hao.

Ishu kamili ipo hivi, Simba walikuwa wamewapita Yanga kwa pointi nane, lakini wakajikuta wakishushwa taratibu mpaka nafasi ya pili na hivyo kuwafanya wapenzi wa soka nchini kuamini kuwa Wekundu wa Msimbazi hao ndio basi tena kwenye mbio za ubingwa.

Yanga walipanda kileleni mwa ligi baada ya kuichapa Stand United mabao 4-0 na hivyo kuwapita Simba kwa pointi nne.

Lakini katika mchezo wao wa Jumamosi iliyopita, Simba walijibu mapigo kwa uishindi wa ugenini dhidi ya Majimaji wa mabao 3-0, hivyo kupunguza pengo la pointi dhidi ya Yanga hadi pointi moja, hivyo kukata ngebe za wapinzani wao hao waliokuwa wakiombea watani wao waangukie pua mjini Songea.

Na sasa wakati Yanga wakiwa safarini kuifuata Ndaya de Mbe ya Comoro watakayocheza nayo Ijumaa katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wanaweza kujikuta wakiwa nyuma ya Simba kwa pointi mbili wakati watani hao watakapokutana katika pambano la kukata na shoka la Ligi Kuu Bara Februari 25, mwaka huu.

Iwapo Simba wataingia uwanjani siku hiyo wakiwa mbele ya Yanga kwa pointi, hali hiyo inaweza kuwapa nguvu ya kushinda na kuongeza pengo la pointi tano zaidi ya watani wao hao na hivyo kuzidi kulisogeza kombe katika Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.

Japo Yanga wamekuwa wakiamini Simba wanaweza kupoteza mchezo kabla ya kukutana nayo baada ya kudhani walishawavunja moyo walipowaacha kwa pointi nne, ukweli ni kwamba kwa morali iliyopo ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kama kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Myanja alivyoliambia BINGWA, ni wazi kuwa Wanajangwani hao wanaweza kujikuta wakiporwa taji la ligi.

Hilo linatokana na ukweli kwamba japo Yanga watakuwa na kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar, lakini hata kama watashinda, haitawasaidia kitu iwapo watakubali kipigo Februari 25 kutoka kwa watani wao hao wa jadi.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wa wikiendi hii na wa Februari 25, Mayanja alisema wana imani watafanya vema kutokana na maandalizi wanayoyafanya.

“Sasa tupo njiani tunarudi Dar es Salaam (wakitokea Songea), ila nina imani tutaweza kufanya vema kwani kwetu kila mechi ni fainali,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -