Sunday, November 1, 2020

YANGA YA MAPESA USICHEZE NAYO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

YANGA wakiwa na pesa mfukoni si timu nzuri kucheza nayo kwani jana wameifanyia kitu mbaya Ndanda FC kwa kuichapa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru na kuchezeshwa na mwamuzi, Erick Onoka kutoka Arusha, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Donald Ngoma aliyetupia mawili, Amissi Tambwe na Vincent Bossou.

Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 40 wakiwa nyuma ya Simba wanaoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 41.
Yanga walianza mchezo kwa kasi huku wakifanya mashambuzi ya nguvu langoni mwa Ndanda  na Ngoma kufanikiwa kupata bao dakika ya tatu kwa kichwa  kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima.

Beki wa Yanga, Juma Abdul, alikosa nafasi ya wazi ya kufunga dakika ya nne  baada ya kupiga shuti la mbali na mpira kutoka nje baada ya kupokea pasi ya mwisho ya Niyonzima.

Yanga waliendelea kufanya mashambulizi ambapo Emmanuel Martin alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya saba baada ya Tambwe kuwachenga mabeki wa Ndanda na kutoa pasi kwa Martin.

Ndanda walifanya shambulizi zuri dakika ya 12, lakini Kigi Makasi alishindwa kufunga mpira wa adhabu baada ya shuti lake kudakwa na kipa wa Yanga,  Deogratuas Munishi ‘Dida’.

Yanga walionekana kutawala mchezo  zaidi, Tambwe alikosa bao dakika ya 19  baada ya kupiga shuti kali kwa mguu wake wa kushoto na kutoka nje ya lango.

Ngoma aliongeza bao la pili dakika ya 20 akimalizia kazi nzuri ya Abdul iliyoanzia kwa Tambwe.

Tambwe alifunga bao la tatu dakika ya 25 baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni.

Bossou aliifunga Yanga bao la nne kwa kichwa dakika ya 88 kutokana na mpira wa kona iliyochongwa na Abdul.Hata hivyo, Ndanda walikosa bao dakika ya 89 baada ya Kigi kupiga shuti, lakini  kipa wa Yanga, Dida alidaka.

Yanga: Deogratuas Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Thaban Kamusoko (dk 70), Juma Makapu/Justine Zulu (dk 60), Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin/Daus Kaseke (dk 78).

Ndanda: Jeremiah Kisubi, Bakari Mtama, Paul Ngalema, Hemed Khoja, Salvatory Ntebe/Ayoub Shabani(dk 38),  Abuu Ubwa, Nassoro Kapama, Salum Telela, Omary Mponda, Riphat Hamis na Kiggi Makasi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -