Wednesday, November 25, 2020

YANGA YAACHA NYOTA WATANO DAR

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

KIKOSI cha Yanga kimeondoka jijini Dar es Salaam jana kwenda mkoani Ruvuma kucheza na wenyeji Majimaji katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayochezwa kesho kutwa huku wakiwaacha nyota watano.

Nyota walioshindwa kuambatana na kikosi hicho ni Donald Ngoma, Justin Zulu, Obrey Chirwa, Emmanuel Martin na Malimi Busungu kutokana na matatizo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Daktari wa Yanga,  Edward Bavu, watawakosa wachezaji katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji kutokana na baadhi yao kuwa majeruhi.

Aliwataja wachezaji ambao ni majeruhi kuwa ni Ngoma na Zulu ambao  wanasumbuliwa na goti na Obrey Chirwa, aliyeumia kabla ya timu hiyo kwenda Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi.

“Ukiwatoa wachezaji hawa wengine ambao wapo kwenye msafara wa kwenda Ruvuma wote wako fiti,” alisema Bavu.

Katika hatua nyingine, Meneja wa timu hiyo, Hafidh  Saleh, alisema licha ya kuwakosa wachezaji  hao, anaamini waliobaki watafanya kazi nzuri.

“Kikosi chetu ni kipana na wanapokosekana wengine bado kinaendelea na makali yake kwa kuwa wapo wanaoweza kuziba pengo la wenzao,” alisema.

Katika hatua nyingine, winga wa timu hiyo, Simon Msuva, bado ana hasira za kukosa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi uliochukuliwa na Azam wiki iliyopita visiwani Zanzibar na anaelekeza nguvu kwa Majimaji.

Wachezaji wa timu hiyo wataingia  uwanjani kama mbogo aliyejeruhiwa baada ya kufungwa mabao 4-0 na Azam katika mchezo wa makundi wa Kombe la Mapinduzi, kisha penalti 4-2 kufuatia sare tasa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba.

Msuva alisema baada ya  kupata matokeo hayo, anahamishia nguvu Ligi Kuu Bara ambao keshokutwa wanakuwa wenyeji wa Majimaji.

“Kwanza niseme wachezaji tulijitahidi kwenye michuano ile ya Mapinduzi,  lakini bahati haikuwa upande wetu, akili zetu tunazielekeza ligi kuu.

Utakuwa mchezo mgumu kwani hata wenzetu watakuwa wamejiandaa vizuri  ila tutahakikisha tunashinda,” alisema Msuva.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -