Wednesday, November 25, 2020

YANGA YAFANYA KWELI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WAANDISHI WETU

MABOSI na benchi la ufundi la Yanga wameuangalia kwa umakini uwezo wa wachezaji wao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar Jumamosi ya wiki iliyopita na kugundua baadhi ya kasoro kadhaa na hivyo kuitana kujadiliana nini cha kufanya kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Yanga wakiwa na kocha wao mpya, George Lwandamina, walijikuta wakifungwa mabao 2-1 mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi.

Awali kabla ya mchezo huo, mashabiki wengi walitarajia kikosi chao kitaibuka na ushindi kutokana na marekebisho ya benchi la ufundi, lakini wakajikuta wakiondoka uwanjani vichwa chini.

Katika mchezo huo, Lwandamina ni kama aliamua kuwachongea wachezaji kwa mashabiki, kwani aliwapa wote nafasi ya kucheza, ambapo hata wale waliokuwa wakilalamika kuwekwa benchi na Hans van der Pluijm, waliingizwa.

Baadhi ya wachezaji walionyesha viwango duni na kuwafanya mashabiki kushangaa, ambapo juzi mabosi wa Yanga waliamua kwenda kukaa kikao cha zaidi ya saa sita katika moja ya hoteli za kifahari Dar es Salaam ili kuona nini wanaweza kufanya wakati huu dirisha dogo la usajili likielekea ukingoni.

Vigogo wa Kamati ya Mashindano, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Samwel Lukumay, walikutana kutathmini juu ya kikosi chao hicho kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa rasmi wiki hii.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga kililiambia BINGWA moja ya mambo ambayo vigogo hao waliyatilia mkazo na kuyajadili kwa kina, ni namna gani wanavyoweza kufanya mapinduzi ya haraka kusajili wachezaji wengine ambao watakuwa na msaada ndani ya kikosi hicho cha Jangwani na hivyo kutimiza ndoto ya mashabiki wao ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na pia kutamba kwenye kipute cha Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo, kiliimbia BINGWA: “Unajua dirisha dogo linafungwa wiki hii, sasa kabla halijafungwa, kuna jambo la kushtukiza linaweza kutokea ndani ya siku mbili hizi.

“Kutokana na kile kilichoonekana juzi katika mchezo dhidi ya JKU, kuna wachezaji wanaweza wakaondoka muda wowote na tukaongeza wengine mapema tu kabla siku ya mwisho ya usajili.”

Mtoa habari huyo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani, alisema kuwa wajumbe wa Kamati ya Mashindano wamelitaka benchi la ufundi kupendekeza wachezaji wa kutemwa na wa kusajiliwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

“Wana-Yanga wasiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa sawa, labda niwape habari njema kuwa kuna kitu kikubwa kitafanyika na watashangaa, uzuri ni kwamba, kila mmoja amejionea mwenyewe ni wachezaji gani hawana msaada ndani ya timu, hivyo wanaletwa watu wa kazi ndani ya siku hizi mbili,” alisisitiza kiongozi huyo wa Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -