Sunday, October 25, 2020

YANGA YAICHEZA MECHI YA SIMBA, URA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

YANGA ni kama vile wameicheza tayari mechi baina ya Simba na URA ya Uganda, itakayochezwa leo baada ya mabingwa hao wa Tanzania Bara jana kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto ya Zanzibar.

Ushindi huo wa Yanga sasa utailazimisha Simba kupata ushindi au sare kwenye mchezo wake wa leo, ili kujihakikishia kukaa kileleni na kukwepa kukutana nao kwenye hatua ya nusu fainali.

Yanga imefikisha pointi sita na bado ina mechi moja dhidi ya Azam, lakini ikionekana kuwa huenda tayari imekata tiketi ya kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuwa wana mtaji mkubwa wa mabao katika michuano hiyo, wakiwa wamefunga mabao nane (8).

Simba hawatakuwa na jinsi isipokuwa kutangulia kukaa kileleni hasa kwa kuzingatia kuwa wapinzani wao wa jadi nao wana uwezekano mkubwa wa kumaliza kileleni lakini hata hivyo kama Yanga itamaliza nafasi ya kwanza Simba watakutana na Azam FC ambayo ina uwezekano mkubwa wa kushika nafasi ya pili kwenye kundi A.

Katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, shujaa wa Yanga alikuwa Simon Msuva, aliyefanikiwa kufunga mabao yote mawili na aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.

Matokeo hayo yameiwezesha Yanga kuongoza kundi B, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa kwanza na timu pekee ambayo inaweza kuifikia Yanga kwenye kundi hilo ni Azam ambayo hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa ikicheza na Jamhuri ya Pemba.

Yanga ambao walionekana kutawala mchezo katika dakika 45 za kwanza, Msuva alifunga bao la kuongoza dakika ya 11 baada ya kumalizia shuti la adhabu lililopigwa na Haruna Niyonzima, kufuatia kuchezewa rafu na mchezaji wa Zimamoto, Hassan Haji, nje ya eneo la hatari.

Baadaye, Yanga walifanya shambulizi zuri dakika ya 13, lakini Emmanuel Martin, alishindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Msuva.

Kabla ya pasi kumfikia Msuva mpira  ulianzia kwa Niyonzima na Martin alikosa umakini huku shuti lake likipaa juu ya lango.

Msuva aliongeza bao la pili dakika ya 21  kutoka mpira wa katikati ya uwanja na kumtoka beki wa Zimamoto, Yussuf Mtuba na kupiga shuti lililokwenda wavuni.

Zimamoto walifanya shambulizi dakika ya 29, lakini Hamad Vuai, alikosa bao la wazi akiwa amewatoka mabeki wa Yanga, Andrew Vincent na Kelvin  Yondani, lakini alijikuta akipiga shuti nje ya lango.

Kipindi cha pili kilianza kwa Zimamoto  kusaka bao, lakini safu yao ya ushambuliaji ilionekana kuwa butu kutokana na kushindwa kutumia nafasi walizopata.

Hata hivyo, Msuva alikosa penalti dakika ya 52 baada ya kipa wa Zimamoto, Mwinyi Hassan Khamis, kupangua shuti lake, lakini pia Msuva akashindwa tena kumalizia mpira uliotemwa na kipa huyo.

Yanga walipata penalti hiyo baada ya Msuva kuchezewa madhambi ndani ya eneo la hatari na beki wa Zimamoto, Hassan Haji.

Msuva angekuwa makini angeweza kuipatia timu yake bao la tatu dakika ya 58, lakini mpira wake wa kichwa ulitoka nje.

Yanga: Deogratius Minishi ‘Dida’, Juma Abdul/Hassan Ramadhan Kessy, Mwinyi Haji, Andrew Vicent, Kelvin Yondan, Justine Zulu, Simon Msuva, Thaaban Kamusoko, Juma Mahadhi/Oscar Joshua, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke na Emmannuel Martin/ Geogrey Mwashiuya.

Zimamoto: Mwinyi Hassan Khamis, Yusuph Ramadhan Mtuba, Hassan Haji Ali/Nyange Othman Denge, Suleiman  Said Juma, Shafii Hassan Rajab/Sleiman Sheha Abass, Hajji Nahodha Haji, Hassan Said Hassan, Makame Hamad Mbwana, Hakim Khamis Ali/Jafari Abdi Rashid, Ibrahim Hamad Hamad na  Hamis Mgeni Vuai.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -