Wednesday, October 28, 2020

YANGA YAIPA FAIDA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM, ZANZIBAR

USHINDI wa Simba dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga, umekuwa ni neema kubwa kwa kocha wa kikosi cha timu hiyo, Joseph Omog na msaidizi wake, Jackson Mayanja.

Kuelekea katika mchezo wao wa fainali leo dhidi ya Azam na mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara, ushindi wa penalti umelizindua benchi la ufundi la Simba ambalo awali halikuwa na mipango ya masuala ya upigaji wa penalti katika programu zao.

Simba walifanikiwa kutinga fainali baada ya kuifunga Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2, katika mchezo wa nusu fainali wa kombe hilo, kufuatia sare tasa ndani ya dakika 90 uliochezwa Jumanne wiki hii usiku kwenye Uwanja wa Amaan.

Omog na Mayanja sasa wameanza programu maalumu ya kuwapigisha penalti wachezaji wao kwa ajili ya mchezo wa fainali, lakini pia kwa tukio lolote la penalti kwenye mechi za Ligi Kuu.

“Mechi ya Yanga imetuzindua, penalti zile zilitokea tu na kila mmoja tunashukuru alijiamini kwa uwezo wake, lakini hili limetupa faida kubwa sana kwani sasa tumeamua kuwa na programu maalumu itakayotuwezesha kuwa na wapigaji maalumu wa penalti kwa Simba,” alisema Omog.

Katika mazoezi ya juzi Jumatano na jana, Omog alianza programu ya kuwafanyisha mazoezi ya viungo huku wakiruka koni, kupigiana mipira na krosi na baadaye penalti zoezi ambalo lilichukua muda mrefu.

Omog alionekana kuridhishwa na Mzamir Yassin, Ramadhani Shiza ‘Kichuya’, Janvier Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Pastory Athanas, James Kotei, Novaty Lufunga, Mohammed Kijiko na Said Ndemla ambao walitumbukiza vyema penalti zao huku wengine akiamua kuendelea kuwanoa zaidi kwa kurudia rudia mikwaju yao baada ya kukosa au kupiga vibaya.

Zoezi hilo la upigaji wa penalti  halikumhusisha beki wa kati wa timu hiyo, Method Mwanjale, aliyekosa wakati wanacheza na Yanga katika mchezo wa nusu fainali.

Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, alisema hawakuwa na programu ya zoezi la kupiga penalti na imefika baada ya Simba kuingia fainali.

Mayanja alisema ilikuwa ni mara chache kwa wachezaji wa timu hiyo kuandaliwa kupiga penalti, lakini wameona umuhimu huo iwapo mchezo wao wa leo mshindi ataamuliwa kwa mikwaju na wao waweze kushinda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -