Monday, November 23, 2020

YANGA YAIPUMILIA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

MABINGWA watetezi Yanga jana wamerejesha matumaini ya mbio za  kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, baada ya kuidunga Ruvu Shooting mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dare es Salaam.

Yanga ambayo ilianza kupoteza matumaini kutokana na kufungwa na Mahasimu wao wa jadi Simba, sasa wamefikisha pointi 52 nyuma ya mahasimu wao Simba wenye pointi 54.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 31 kwa njia ya penalti, baada ya mwamuzi Ahmed Simba kuamuru ipigwe kufuatia beki wa Ruvu kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Emanuel Martin aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Deus Kaseke, ameifungia Yanga bao la pili dakika za majeruhi kwa kichwa kwa kumalizia krosi safi ya Msuva.

Yanga walianza mchezo wa jana kwa kasi ambapo dakika ya tatu mshambuliaji Godfrey Mwashiuya alipoteza nafasi nzuri ya kufunga wakati aliposhindwa kuunganisha vyema mpira wa krosi iliyochongwa na Amissi Tambwe.

Dakika ya sita, mshambuliaji wa Ruvu, Abrahman Mussa, alifanya shambulizi kali akiunganisha krosi iliyopigwa na Damas Makwaya, lakini shuti lake linaokolewa na kipa wa Yanga, Deogratias Munishi ‘Dida’.

Yanga ambao kwa kipindi chote cha kwanza wanafanya mashambulizi mara kwa mara kwenye lango la Ruvu, lakini ukuta wa timu hiyo ulikuwa imara na kuokoa hatari langoni kwao.

Dakika ya 20 straika Obrey Chirwa  anaikosa nafasi nzuri ya kuifungia Yanga bao baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Ruvu, Bidii Hussein, kufuatia krosi maridadi ya beki wa kulia Hassan Kessy.

Dakika ya 44, Yanga walipata pigo baada ya mwamuzi Simba kutoka Kagera kumuonyesha kadi ya pili ya njano Obrey Chirwa na kutoka nje kwa kadi Nyekundu kwa utovu wa nidhamu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 57, Amissi Tambwe nusura aiongezee timu yake bao kama angemalizia viziri krosi ya Msuva.

Ruvu walionekana pia kutulia zaidi na kuwasumbua Yanga ambapo mara kadhaa washambuliaji wake walifika langoni kwa Yanga lakini hawakuwa na utulivu wa kumtungua kipa Dida wa Yanga.

Yanga licha ya kucheza pungufu kwa kipindi chote cha pili, imetengeneza nafasi nyingi kipindi cha pili ambapo dakika ya 84, Msuva anapewa krosi na Haji Mwinyi ambapo alipiga kichwa lakini mpira ulitoka nje.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -