Sunday, October 25, 2020

YANGA YAISHTUKIA SIMBA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

YANGA imeshtukia janja ya nyani inayofanywa na Simba ili kuwapora taji la Ligi Kuu Tanzania Bara na kocha wa klabu hiyo ya Jangwani, George Lwandamina, kuamua kuongeza dozi ya mazoezi.

Lwandamina anafahamu kwamba kocha wa Simba, Joseph Omog, atakuwa na mikakati ya kufanya awezalo kuhakikisha anakiandaa kikosi chake ili kiweze kuendelea kupata matokeo mazuri ambayo yatawezesha kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Kwa kulitambua hilo, Lwandamina amewaongezea wachezaji wake  mazoezi ya stamina  yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,  wakati huo wakijiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui utakaochezwa Jumapili.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Lwandamina alitumia muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kutengeneza mabao, kuzuia na kumiliki na mpira.

Ambapo washambuliaji wa timu hiyo, Amis Tambwe, Juma Mahadhi, Malimi Busungu na Athony Matheo walipewa jukumu la kupasia mabao nyavuni.

Lwandaminia alitumia dakika 30 kuwafua Tambwe, Haruna Niyonzima na Mahadh ili kuziba pengo la Donald Ngoma ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 45 wakifungwa na Yanga wenye pointi 43.

Pamoja na mazoezi hayo, pia Lwandamina aliwanoa wachezaji wake namna ya kupiga penalti kutokana na kutolewa kwenye michuano mbalimbali linapokuja suala la matuta.

Kwa sasa Yanga wanajiandaa na mchezo huo wa Mwadui pamoja na mtanange mwingine wa Ligi ya Mabinwga Afrika dhidi Ngaya de Mbe, utakaochezwa kati ya Februari 10 au 12 mwaka huu nchini Comoro.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -