Wednesday, October 21, 2020

Yanga yaisogelea simba kileleni

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA,

YANGA wamezidi kuwakaribia Simba kileleni baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva na Haruna Niyonzima, wakati bao la Ruvu Shooting lilifungwa na Abrahman Mussa.

Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 33, ikiwa ni tofauti ya pointi mbili na Simba, ambao wako kileleni kwa pointi 35, baada ya timu zote kucheza mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Ruvu Shooting walianza kupata bao la kuongoza dakika ya saba, lililofungwa na Abrahman, baada ya kumalizia kazi nzuri ya Fully Maganga,  baadaye Msuva aliisawazishia timu yake dakika ya 31,  baada ya Haruna Niyonzima kumlamba chenga beki wa Ruvu, Mau Bofu na kutoa pasi kwa mfungaji.

Kabla ya kusawazisha bao hilo, Yanga walitengeneza nafasi nyingi, lakini washambuliaji wao, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Amis Tambwe walionekana kukosa umakini katika kufunga.

Mwamuzi wa mechi hiyo, Mathew Akrama kutoka Mwanza, alimwondoa kwenye benchi Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, dakika ya 50 baada ya kupishana kauli.

Niyonzima, ambaye alionekana kuwa nyota wa mechi ya jana, alifunga bao la pili dakika ya 56 kwa shuti la mbali, baada ya kupokea pasi ya Ngoma, ambaye kabla alijaribu kufunga, lakini shuti lake likazuiliwa na kisha akarudisha pasi nyuma ambayo ilimkuta Niyonzima, aliyeachia shuti kali lililojaa wavuni.

Ngoma alifanya kazi nzuri dakika ya 69 na kutoa pasi kwa Msuva, lakini alishindwa kufunga baada ya mabeki wa Ruvu kuondoa hatari hiyo.

Ruvu Shooting walifanya shambulizi zuri dakika ya 73, lakini  Issa Kanduru alishindwa kumalizia krosi ya Mussa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -