Saturday, October 31, 2020

YANGA YAITANGAZIA MAAFA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WAANDISHI WETU


UBORA na upana wa kikosi cha Simba ulilitia presha benchi la ufundi la Yanga na kuanza kuwafungia kazi nyota wao ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza ili kuongeza uwezo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba msimu huu wamefanya usajili wa aina yake kwa kunasa nyota wenye uzoefu kwa ajili ya michuano mbalimbali na kuonekana kuwa tishio tofauti na mahasimu wao Yanga ambao wameendelea kusuasua kwenye usajili.

Lakini baada ya benchi la ufundi kufanyia tathmini, limeamua kumfua kila mchezaji ndani ya kikosi hicho na kuhakikisha anakuwa na makali ili kukabiliana na mikikimikiki ya Ligi Kuu msimu huu na mahasimu wao Simba.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema amekiangalia kikosi chao na kugundua si kipana na hakina ubora kama cha wapinzani wao, hivyo wamelazimika kuwavalia njuga wachezaji wao kila mmoja kwa nafasi yake.

Ili kuhakikisha wachezaji wao wanakuwa fiti zaidi, Mwandila aliwahenyesha mno wachezaji wake kwa kuwapigisha tizi la kufa mtu ili kuwajengea stamina na pumzi ya kutosha kupambana.

Katika mazoezi yaliyofanywa juzi na jana asubuhi, Mwandila alionekana akiwakimbiza wachezaji hao ambao hawakupata nafasi ya kuitwa kwenye timu zao za taifa.

Akizungumzia mazoezi hayo, Mwandila alisema yanalenga kuiandaa Yanga mpya itakayokuwa na kikosi kipana kilichokamilika kila idara.

Mbali na kuwapa mbinu za mazoezi, Mwandila alisema Jumapili watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya African Lyon kwa ajili ya kuangalia walichofanya kwenye mazoezi kama yameeleweka.

“Tupo kwenye maandalizi ya kujenga kikosi kitakachokuwa na ushindani, hivyo mechi dhidi ya African Lyon tutaitumia kwa ajili ya kuona ni namna gani wachezaji wameelewa tulichokifanya,” alisema Mwandila.

“Kila mchezaji anapaswa kujituma ndio maana nimegawa majukumu kwa kila mchezaji wa timu hii, atakayeingia uwanjani ahakikishe tunapata ushindi.”

Yanga hadi sasa wamecheza mechi moja pekee ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda mabao 2-1, huku wakitarajiwa kushuka dimbani tena Septemba 16, mwaka huu dhidi ya Stand United na Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, kwa sasa Yanga akili zao wamezielekeza Ligi Kuu ili waweze kurejesha taji hilo ambalo msimu uliopita liliporwa na Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -