Sunday, November 1, 2020

YANGA YAITIKISA RAYON

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI


KIKOSI cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini leo usiku, kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Rayon Sport.

Yanga ambayo inaburuza mkia Kundi D ikiwa na pointi nne, Jumatano itajitupa kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kukamilisha ratiba ya michuano hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema jumla ya wachezaji 20 watakuwa katika msafara huo wakiongozana na viongozi wa benchi la ufundi.

Alisema timu hiyo itaondoka saa 6:00 usiku kwa ndege ya Shiriki la Ndege la Rwanda, wakitarajiwa kufika nchini Rwanda saa 8:00 au 9:00 usiku.

“Maandalizi yamekamilika, timu itaondoka kesho usiku ikiwa na wachezaji 20 na viongozi kadhaa wa benchi la ufundi kwa ndege ya Rwanda Airways,” alisema Hafidh.

Hafidh alisema kuna baadhi ya wachezaji kama Juma Abdul na Juma Mahadhi, watakosekana kwenye safari hiyo kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambapo Abdul aliumia katika mchezo dhidi ya USM Alger huku Mahadhi akiumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Wakati Yanga ikiwakosa nyota wake hao wawili ambao ni majeruhi, Rayon pia itawakosa wachezaji wake watano kutokana na sababu tofauti.

Rayon watamkosa mlinda mlango wao, Kassim Ndayisenga, Yannick Mukunzi na Mbondi Christ, waliopewa adhabu na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa madai ya kuchochea vurugu zilizoibuka baada ya mechi ya marudiano dhidi ya USM Alger nchini Algeria.

Rayon Sports pia itamkosa kiungo wake wa kati, Pierre Kwizera, aliyekataa kuichezea timu yake mechi hiyo baada ya kusajiliwa na klabu ya Daraja la Kwanza Oman.

Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliviera, alikuwa akimhitaji Kwizera baada ya kuwakosa viungo wawili, nahodha wa sasa, Manzi Thierry na Niyonzima Olivier Seif, wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Kwizera ambaye alikuwa nahodha wa Rayon Sports, alitarajiwa kufika Kigali juzi lakini amekataa kuitika wito wa kocha na kuamua kurudi nchini Oman.

Kitendo cha kuwakosa wachezaji hao kumewafanya Rayon kuwa na hofu, huku mshambuliaji mpya wa Yanga, Herieter Makambo ambaye katika mechi zake mbili za mwisho ikiwamo ile ya mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger na ule wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Mtibwa Sugar zote ametingisha nyavu.

Kasi hiyo ya Makambo na kazi nzuri ya kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, imeifanya Rayon kuingiwa hofu kubwa wakihofia kukumbana na kipigo kama kile cha USM Alger ambao walichapwa mabao 2-1.

“Rayon wamekuwa na hofu sana, wamesikia habari za Makambo na kipigo cha USM Alger ndio kimezidi kuwachanganya, wakihofia kuwa wanaweza kufungwa na wao hasa baada ya kuiona timu hiyo ikiwa vizuri,” kilisema chanzo hicho cha karibu na benchi la ufundi la Rayon.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -