Thursday, December 3, 2020

YANGA YAWAMALIZA WAARABU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

YANGA sasa wamejanjaruka na wanaweza kufanya kweli kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger ya Algeria, kwani kwa muda mfupi tu wamegundua fitina na mbinu za Waarabu hao.

Baada ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, timu hizo zilishindwa kufungana mjini Lusaka na Zanaco kunufaika na goli la ugenini na kusonga mbele.

Kwa matokeo hayo Yanga wameangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo droo ya juzi Jumanne ya mechi za kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo imewakutanisha na Mouloudia Club d’Alger (MC Alger).

Timu hizo zitacheza mechi ya kwanza kati ya Aprili 7 hadi 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku ile mechi ya marudiano ikitarajiwa kufanyika Aprili 14 hadi 16 mwaka huu Uwanja wa Omar Hamad mjini Algiers, Algeria.

Kufuatia matokeo mabaya wanayoyapata Yanga mara kwa mara kwenye michuano ya kimataifa hasa wanapokutana na timu za Kiarabu, safari hii klabu hiyo ya Jangwani wamejipanga kuhakikisha wanamaliza fitina zao na tayari wameshamnasa mbaya wao kwenye mechi hizo mbili za hatua ya mtoano ambaye  ni beki wa kulia na nahodha wa MC Alger, Abderrahmane Hachoud.

Pamoja na mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Algeria, Hachoud kucheza nafasi ya beki wa kulia, lakini ni mhimili mkubwa katika kikosi hicho cha MC Alger na mabao yake yameisaidia timu yake kuitoa Bechem United ya Ghana na Renaissance kutoka Chad na kuweza kuingia katika hatua hiyo ya mtoano.

Chanzo cha ndani kutoka timu ya Yanga, kimesema klabu hiyo ya Jangwani imeanza mikakati yao mapema tofauti na siku zote jambo ambalo linaifanya wagundue mambo kadhaa muhimu dhidi ya wapinzani wao.

“Safari hii ni mwendo wa kupangua fitina za Waarabu, kwanza tunajua kwamba kuna watu wao ambao watataka kupata mikanda ya timu yetu na wengine kuja kwenye mechi tutakazocheza, hapo imekula kwao. Lakini sisi tumekuwa wajanja kidogo mara baada ya kutangazwa ratiba wao walikuwa na mechi tumeiona, lakini tumepata pia mechi kadhaa walizocheza,” alisema mtoa habari wetu.

“MC Alger wanacheza kwa kasi sana na Hachoud anakimbia upande wa kulia, unaweza ukadhani ndiye winga wao kumbe ni beki, yaani ndiye mchezaji mbaya kwenye kikosi hicho.

“Huyu wanamwita Dani Alves kule kwao, ndiye anayetengeneza mashambulizi mengi kulilo wengine, hupiga krosi ‘dongo’ ambazo mara nyingi huzaa matunda aidha washambuliaji wao wafunge ama mabeki wajifunge wenyewe.

“Ukiachana na kasi yake, pia ndiye mtaalamu wa mipira ‘iliyokufa’, ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti hata akiwa anakimbia anaweza akapiga na hutumia njia hiyo kufunga na kusaidia sana mashambulizi kwenye kikosi chake,” alisema.

Pia chanzo hicho kililiambia BINGWA jana kwamba, jambo lingine ambalo vibosile wa Yanga wamegundua ni mfumo unaotumiwa na kocha wa kikosi hicho, Kamel Mouassa wa 4-1-3-2, ambao hujaza viungo wengi katikati ya uwanja na huwapa nafasi ya kushambulia kwa kushtukiza.

“Mfumo wao huo nao ni moja ya kitu kikubwa kilichoonekana kuwa ni tishio, MC Alger, pia ndio unaompa jeuri sana Hachoud,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -