Tuesday, November 24, 2020

YANGA YAMLETA CHAILA DAR

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM,

KUFUATIA usumbufu wanaoupata Yanga kutoka kwa mshambuliaji wao, Donald Ngoma, katika siku za hivi karibuni, uongozi wa klabu hiyo umeamua kutafuta mbadala wake ambaye ni kiungo wa Zambia, Misheck Chaila wa Zesco United.

Ngoma amebakisha miezi mitatu katika mkataba wake wa sasa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kukiwa hakuna dalili zozote za yeye kuongeza mkataba mpya.

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimesema tayari uongozi umempa kocha wao, George Lwandamina, jukumu la kusaka mchezaji ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi zote za kiungo kwa ajili ya msimu ujao.

Kutokana na Chaila kuwemo kwenye orodha ya wachezaji waliokuwa wanatakiwa na Lwandamina wakati anaingia klabu ya Yanga, ikashindikana kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba mrefu na Zesco, safari hii mambo yanakwenda vizuri baada ya kocha huyo kuanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo.

“Usajili wa Chaila ulishindikana wakati wa dirisha dogo na uongozi wa Zesco haukuwa tayari kumwachia mchezaji huyo kwa kuwa walikuwa wanashiriki ligi kuu na Ligi ya Mabingwa barani Afrika, lakini kwa sasa Lwandamina ameanza mazungumzo na mambo yanakwenda poa na nyota huyo atajiunga na kikosi hicho usajili wa dirisha kubwa,” kilisema chanzo hicho cha habari.

BINGWA lilimtafuta kiungo huyo kwa simu nchini Zambia, ambapo alisema baada ya mkataba wake na Zesco kumalizika, hataongeza mkataba mwingine kwani tayari ameshapata ofa ya kuja kucheza Yanga kwa msimu ujao.

Alisema amekuwa na mawasiliano mazuri na kocha wake, Lwandamina ambaye alimfundisha alipokuwa anainoa Zesco.

“Ni kweli nitakuja kucheza soka Tanzania baada ya mkataba wangu kumalizika mwishoni mwa msimu huu, nitacheza Yanga ambayo anafundisha kocha Lwandamina,” alisema Chaila.

Wakati huo huo kuna wachezaji wawili wanaohusishwa kujiunga na Yanga kwa msimu ujao, ambao ni kiungo wa Mbeya City, Rafael Daudi pamoja na Salim Hoza kutoka Mbao FC ya jijini  Mwanza.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Mbao, Richard Athanas, amefunguka kuhusu mchezaji wao huyo kutakiwa na Yanga,  akisema wao pia  wanazisikia taarifa hizo za kutakiwa kwa Hoza, lakini hadi sasa hakuna ofa iliyokuja mezani kwao.

“Tumezisikia taarifa hizo, ila hatuwezi kuzungumzia vitu ambavyo si rasmi, Hoza ana mkataba na Mbao na kama kutakuwa na suala lolote litawekwa wazi,” alisema Athanas.

Mbali na mchezaji huyo, pia vibopa wa Yanga wameanza harakati za kumnasa kinda wa Azam FC, Gadiel Michael, kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya ulinzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -