Wednesday, October 28, 2020

YANGA YAMSHITAKI KOTEI TFF

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI


 

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikieleza malalamiko yake juu ya kitendo cha beki wa Simba, James Kotei, kumpiga beki wao, Gadiel Michael kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha timu hizo Jumapili iliyopita.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 0-0, vipo vipande vya picha vikimwonyesha beki huyo wa Kimataifa wa Ghana akimpiga mchezaji mwenzake, lakini mwamuzi Jonesia Rukyaa hakuliona tukio hilo, hivyo hakuadhibiwa.

Akizungumza na wanahabari jana, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema tayari wameandika barua hiyo kwa TFF wakisubiri uamuzi utakaotolewa na wahusika.

“Tunamfahamu James Kotei ni mchezaji mwenye nidhamu sana, sijawahi kusikia kafanya kitendo chochote cha utovu wa nidhamu, pengine siku ile ilikuwa ni presha ya mchezo, lakini alipaswa kumuomba radhi mwenzake (Gadiel) baada ya mechi.

“Lakini hata kama alishindwa kufanya hivyo baada ya mchezo angetumia hata kwa kuandika kwenye ukurasa wake katika mitandao ya kijamii, kuonyesha haikuwa kusudio lake kama ambavyo nyota wengine huwa wanafanya, badala yake ameendelea kukaa kimya, hivyo kama uongozi wa Yanga tumeamua kuchukua hatua ya kuishitakia TFF, wao ndio wenye maamuzi,” alisema Ten.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -