Monday, January 18, 2021

Yanga yapata no. 6 hatari

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

HATIMAYE tatizo la kiungo namba sita lililokuwa likiikabili Yanga, litapata tiba muda si mrefu iwapo mkakati wa timu hiyo kumtwaa Misheck Chaila anayekipiga Zesco ya Zambia, utatiki.

Mpango huo wa Yanga wa kumsajili kiungo huyo mkabaji mwenye kila sifa ya kuitwa kiungo, umekuja siku chache baada ya klabu hiyo ‘kumtupia ndoano’ kocha wa mabingwa hao wa Zambia, George Lwandamina.

Ikumbukwe kuwa BINGWA lilikuwa gazeti la kwanza kuripoti juu ya mpango wa Yanga kumtwaa Lwandamina katika toleo la Jumamosi iliyopita, Oktoba 8, mwaka huu ambapo kocha huyo tayari amelithibitishia gazeti dada ya hili, DIMBA kuwa ni kweli mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanamtaka.

Wakati habari ya mjini kwa sasa iliyobamba katika vyombo vya habari ikiwa ni suala la Lwandamina aliyeibuliwa na BINGWA, gazeti hili limepata habari mpya kuwa Yanga imepiga hatua zaidi katika mkakati wake wa kukiimarisha kikosi chao kwa kuingia katika anga za Chaila.

Kama ilivyokuwa kwa habari juu ya Lwandamina, gazeti hili jana lilinasa habari kutoka Zambia kwamba Chaila anajiandaa kutua Yanga na tayari ameanza kuipeleleza timu hiyo kupitia wachezaji wenzake wanaoifahamu.

Akizungumza na BINGWA jana, mmoja wa rafiki wa mchezaji huyo huko Zambia, alisema: “Ameniuliza habari juu ya Yanga nami nikamfahamisha kwasababu naifahamu vizuri tu. Alifurahi kusikia Yanga ni timu kubwa Tanzania na yenye mashabiki wengi na ameonyesha wazi nia ya kuja huko.

“Nilipomuuliza kwanini ameiulizia Yanga na si Simba, alisema kuwa timu hiyo inamtaka na ameonyesha anatamani kuja huko, hasa akifahamu kuna Mzambia mwingine anayefahamika kwa jina la Chirwa (Obrey) anayechezea Yanga.”

Alipoulizwa juu ya uwezo wa mchezaji huyo, rafiki huyo wa Chaila (jina kapuni), alimmwagia sifa akisema kuwa kiungo huyo ana uwezo wa hali ya juu na ni king’ang’anizi hasa ambaye anaamini akitua Yanga, ataisaidia mno timu hiyo.

Baada ya kutonywa juu ya hayo, BINGWA liliamua kumchimba zaidi Chaila kupitia mitandao mbalimbali na kubaini kuwa miongoni mwa sifa alizonazo ni pamoja na kupora mipira kwa kila aina ya mbinu, ikiwamo ile maarufu kwa jina la ‘kuingia uvunguni’, yaani kuteleza, kupora mipira miguuni mwa mpinzani wake.

Pia, Chaila ni mtaalamu wa ‘kukata umeme’, yaani kutibua mipango ya timu pinzani zinapotafuta mabao, aidha iwe kwa kuingilia pasi au kuzuia njia kama anavyofanya kiungo mkabaji wa Arsenal, Francis Coquelin, nyota mpya wa Chelsea, N’Golo Kante ambaye msimu uliopita alikuwa Leicester City, zote za England.

Chaila ndiye kiungo aliyekuwa kikwazo kwa Al Ahly wakati timu hiyo ya Misri ilipovaana na Zesco katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, kuanzia mchezo wa kwanza nchini Zambia hadi ule wa ugenini nyumbani kwa Waraabu hao.

Kati ya wachezaji wa Al Ahly ambaye hatamsahau Chaila, yupo mshambuliaji hatari wa timu hiyo na ile ya Taifa ya Misri, Abdallah Said ambaye alijikuta akishindwa kufurukuta mbele ya kiungo huyo Mzambia mwenye umbo la wastani, akiwa ni mrefu wa kutosha.

Kwa kipindi kirefu, Yanga imejikuta ikiwa na tatizo katika nafasi ya kiungo namba sita kiasi cha kumtumia Mbuyu Twite ambaye hata hivyo si mchezaji sahihi wa nafasi hiyo.

Kwa vipindi tofauti, Yanga imejaribu kuwatumia Said Juma Makapu, Pato Ngonyani, Thaban Kamusoko, Salum Telela (ambaye kwa sasa yupo Ndanda FC) na wengineo kadhaa katika nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, lakini wote walionekana kufiti.

Na sasa ni wazi ujio wa Chaila, utakuwa umetibu tatizo hilo sugu linalowakabili Yanga.

BINGWA jana lilihaha kuwatafuta viongozi wa Yanga kuzungumzia juu ya ujio wa Chaila, lakini hakuna aliyepatikana japo mmoja wa maofisa walio karibu na timu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, alisema: “Nyie BINGWA wachokozi sana, juzi mmetuvujishia stori yetu ya ujio wa Kocha Lwandamina, leo mmeibuka tena….hivi nani anawavujishia siri zetu?”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -