Friday, October 30, 2020

YANGA YAPIGA MTU MKONO MORO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS, MOROGORO


 

YANGA wametoa kipigo cha mabao 5-1 kwa timu ya Morogoro Tanzanite, katika mchezo wao wa kwanza wa kirafiki tangu walipoanza kambi yao mjini hapa, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Wanajangwani hao wanatarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu Bara Agosti 22, mwaka huu, kwa kuvaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, uliopo mjini hapa.

Lakini kabla ya kupepetana na Mtibwa, Yanga watakutana na USM Alger wiki ijayo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wao wa tano wa michuano hiyo ya Afrika hatua ya makundi.

Katika mchezo huo wa jana wa kujipima nguvu uliochezwa Uwanja wa Chuo cha Biblia mjini hapa, mabao ya Yanga yalifungwa na Mrisho Ngassa, Herietier Makambo, Deus Kaseke, Pius Buswita na Emmanuel Martin.

Katika mabao yote, lililofungwa na Kaseke lilikuwa ni bab kubwa, kwani baada ya kupokea mpira wa juu kutokana na krosi ya Haji Mwinyi, Makambo alimtengea mfungaji bonge la pande kwa kifua na kiungo huyo kutikisa nyavu za wapinzani wao hao.

Bao la Morogoro Tanzanite Academy liliwekwa kimiani na Omari Jaribu ‘Samatta’, baada ya kutumia vema kosa la Kakolanya, aliyeteleza wakati wa kuondosha hatari langoni mwake na mpira kumkuta mfungaji.

Mchezo huo angalau umetoa picha ya kikosi cha kwanza cha Yanga, lakini pia vita ya namba ilivyo kubwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo, zaidi ikiwa ni safu ya kiungo.

Kikosi kilichoanza kiliwahusisha kipa Benno Kakolanya, Juma Abdul, Mwinyi, Vincent Andrew ‘Dante’,  Shaibu Abdallah ‘Ninja’, Feisal Salim ‘Fei Toto’, Mrisho Ngassa, Rafael Daudi, Makambo, Buswita na Kaseke.

Wachezaji wote walionyesha kiwango kizuri, huku kila mmoja akionekana kufanya vema kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kikosi cha kwanza.

Kwa upande wa Ngassa, kama ilivyo kawaida yake, alikuwa akihaha kila upande, akiwa mwepesi katika kupokea mipira na kuiachia kabla ya ‘kufungua’ tayari kupasi tena.

Kaseke naye alikuwa akihaha kama Ngassa, akionekana kurejea Jangwani kwa moto kama vile ametumwa na ‘kijiji’ kuikomboa timu hiyo.

Fei Toto, ambaye amejitambulisha kama mchezaji atakayewateka mno mashabiki na wanachama wa Yanga msimu huu, jana alionyesha makeke yake yaliyomfanya kutua Jangwani na kuwapagawisha mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo.

Kati ya mambo yaliyowavutia wengi, ni uwezo wake wa kupokea mpira kama sumaku, kupiga mapande ya maana na zaidi kufunguka kwa kasi kuomba mipira kiasi cha kuwarahisishia kazi mabeki pale walipobanwa wasijue wapi pa kupeleka mpira.

Makambo, ambaye wapenzi wa Yanga wamekuwa na shauku ya kuona kiwango chake,  alicheza vizuri tu, akiwa ni fundi wa ‘kuficha’ mpira, japo anaonekana bado hajachangamka.

Bila shaka kadri siku zinavyokwenda, anaweza kuwa moto wa kuotea mbali kwa mabeki kutokana na ‘utajiri’ alionao wa nguvu, akili ya mpira na shabaha anapokuwa mbele ya goli.

Kwa upande wa makipa, bado kuna ushindani wa namba baina ya Kindoki Nkizi na Kakolanya, ambaye anaonekana kurejea kwa kasi akitaka kutwaa nafasi ya kipa namba moja wa timu hiyo.

Kwa ujumla, wachezaji wote wameonekana kujituma, kwani hata wale walioingia kipindi cha pili, Nkizi,  Juma Mahadhi, Gadiel Michael, Cleophace Sospeter, Pato Ngonyani,  Said Juma Makapu, Yusuph Mhilu/Said Mussa, Japhary Mohammed/Maka Edward, Amissi Tambwe, Thaban Kamusoko na Matheo Anthony/Baruan Akilimali.

Yanga wanatarajiwa kuendelea na mazoezi leo na wikiendi hii watamenyana na Mawezi Market FC ya hapa kwenye Uwanja wa Jamhuri, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kumuaga nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, aliyestaafu na kupewa cheo cha Meneja wa Timu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -