Sunday, January 17, 2021

YANGA YATOSA WAWILI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA SHARIFA MMASI

YANGA wajanja sana asikwambie mtu! Uongozi wa klabu ya Yanga umeshtuka na kuepuka kuingia chaka baada ya kuamua kuwatosa fasta wachezaji wa kigeni wawili waliokuwa wakifanya majaribio na kumbakiza Issa Anifewoshe walioonyesha nia ya kumsajili.

Wachezaji hao ambao walikuwa kwenye majaribio, ni Mnigeria Tony Okoh pamoja na Mcameroon Fernando Bongyang, ambao wamekatiwa tiketi za ndege na kurejereshwa makwao, lakini benchi la ufundi la Wanajangwani hao likiongozwa na Kocha  Mkuu George Lwandamina, limeona viwango vyao ni vya kawaida sana na kuwaambia viongozi waangalie namna ya kuwaondoa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa, alithibitisha klabu yake hiyo kuachana na wachezaji hao akidai kuwa benchi la ufundi ndilo lililopendekeza jambo hilo na kwamba, wao kama viongozi wanatekeleza tu.

“Kama mnavyojua kwamba tulikuwa na wachezaji wawili wa kigeni waliokuwa wakifanya majaribio, mmoja kutoka Nigeria na mwingine Cameroon, taarifa ni kwamba benchi la ufundi limeona wawili hao hawana vigezo vya kuichezea Yanga hivyo tumeamua kuachana nao.

“Tayari yule Mnigeria (Okoh) tumeshamkatia tiketi na ameshaondoka na sasa tunamfanyia utaratibu huyo Mcameroon (Fernando), ili naye aondoke, hatutaki kabisa msimu huu kusajili watu ambao watatuletea shida mbele ya safari ndiyo maana tuko makini sana,” alisema.

Wakati wawili hao wakiondolewa, nyota inaonekana kung’ara kwa beki kisiki Mnigeria Anifowoshe, ambaye pia yupo kwenye majaribio kwani kutokana na uwezo mkubwa anaouonyesha mazoezini, ana kila dalili ya kusajiliwa.

Beki huyo ametua nchini hivi karibuni kwa ajili ya majaribio, ambapo kuna kila dalili akasajiliwa kutokana na uwezo wake mkubwa anaouonyesha ndani ya uwanja na kutokana na shida ya beki wa kati waliyonayo, wakifanikiwa kunasa saini ya Mnigeria huyo watakuwa wamelamba dume.

Yanga wanayo shida kubwa ya beki wa kati hasa baada ya kuachana na Vincent Bossou, huku pia Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, umri ukiwatupa mkono hivyo wanatakiwa kusajili mtu wa kazi ambaye anaweza kukabiliana vizuri na washambuliaji wenye uchu wa mabao kama Emmanuel Okwi wa Simba.

Katika hatua nyingine, Mkwassa alisema kiungo wao rasta Kabamba Tshishimbi, anatarajiwa kuwasili mchana wa leo ambapo ataambatana na kikosi hicho kwenda Pemba, Jumapili ya wiki hii kuweka kambi ya kuwawinda watani zao wa jadi Simba, mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 23, mwaka huu.

Pia Katibu huyo kwa niaba ya uongozi wote wa Yanga, wameishukuru Azam FC kwa kukubali kumwachia beki wao wa kushoto Gadiel Michael, kujiunga na Wanajangwani hao.

Kuhusu mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting, Mkwassa alisema mchezo huo hautachezwa tena Uwanja wa Uhuru kama walivyosema awali na badala yake utakuwa Uwanja wa Chamazi, kutokana na Uwanja wa Uhuru kuwa na shughuli za kiserikali huku akiwaomba mashabiki wao kujitokeza kwa wingi

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -