Thursday, December 3, 2020

YANGA YATUMA TIMU YA ‘MAUAJI’ ALGERIA  

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

 

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY


 

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, sasa wanataka kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwa kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kuiondoa MC Alger ya Algeria katika mchezo wa marudiano utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii, huko Algeria.

Yanga wanafahamu kwamba ushindi huo ni mwembamba na hivyo tayari wamesuka mkakati kabambe wa kuhakikisha wanaandika historia mwaka huu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na kuitoa timu za Ukanda wa Kaskazini.

Kutokana na hilo na kufahamu juu ya fitina za timu za huko Kaskazini hasa katika nchi za Kiarabu, Wanajangwani hao wameunda timu maalumu itakayotangulia mapema kwa lengo la kuweka mazingira sawa kuelekea katika mchezo huo.

Yanga wanatarajia kurudiana na timu hiyo Ijumaa, kwenye Uwanja wa Stade 5 Juillet 1962 mjini Algiers, baada ya juzi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, alisema ingawa ni mapema mno kuzungumzia mipango yao kuelekea mchezo wa marudiano, lakini wamejipanga kuhakikisha wanazikabili fitina za Waarabu hao.

“Leo (jana) ni Jumapili, ni mapema sana kuzungumza tutafanya nini kule au tumejipangaje, lakini fitina zote za Waarabu tunazijua na tuna imani tutafanya vizuri,” alisema Mkwasa.

BINGWA linazo taarifa za ndani kutoka Kamati ya Mashindano ya timu hiyo wakishirikiana na Kamati ya Utendaji kwa pamoja wamepanga kutuma ujumbe wa watu wanne utakaoondoka kesho kwenda mjini Algiers kwa ajili ya kuandaa mazingira mazuri ya timu itakapofikia, hoteli watakayolala na usafiri wa ndani watakoutumia.

“Tunajua hii ni vita kubwa, jamaa watahitaji ushindi kwa namna yoyote ile, kwa hiyo na sisi lazima tujipange vyema, hawa jamaa ni hatari sana katika suala zima la hujuma za nje ya uwanja kama mambo yataenda vizuri lazima tuondoke mapema,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wake mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, Siza Agustino, aliliambia BINGWA jana kuwa walikuwa na kikao kizito kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo na Kamati ya Mashindano ya timu hiyo kupanga mikakati mizito ya namna ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo na kutinga hatua ya makundi.

“Tupo katika kikao hapa klabuni, sisi kama Kamati ya Utendaji na Mashindano, mipango ni mzito kidogo siwezi kukwambia sasa hivi kwa sababu bado hatujamaliza kikao ila nitafute baadaye,” alisema Siza.

Alisema timu itaendelea na mazoezi yake leo katika Uwanja wa Chuo cha Polisi na Alhamis itaondoka kuelekea Algeria tayari kwa ajili ya mtanange huo wa marudiano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -