Saturday, October 31, 2020

MATUKIO YA MICHEZO MEI 2016; YANGA YATWAA MATAJI YOTE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

KADIRI siku zinavyokwenda ndivyo tulivyobakisha siku chache kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017, ambapo yapo mashindano mengi ndani na nje ya nchi tunayotarajia kufanya vyema na kuondokana na usemi ‘Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu’. BINGWA leo linamulika matukio ya michezo yaliyotokea Mei 2016 ikiwa ni mwendelezo wa kujikumbushia matukio muhimu yaliyojiri mwaka huu.

*Yanga baba lao Bara

Yanga imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara baada ya mahasimu wake Simba kufungwa 1-0 na Mwadui katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ushindi wa Simba ungewachelewesha Yanga kutwaa ubingwa huo zikiwa bado mechi mbili zimebaki ligi kumalizika, lakini alikuwa Jamal Mnyate aliyezima ndoto za Simba na wakati huo huo kuipa Yanga ubingwa.

Yanga ilimaliza ligi ikiwa na pointi 73 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Azam FC yenye pointi 64 na Simba ikimaliza na pointi 62.

*Tanga! Kunani paleee…

Historia ya aina yake imeandikwa Ligi Kuu Bara baada ya timu zote kutoka Tanga kushushwa kutokana na matokeo mabovu waliyopata msimu wa 2015/16.

Coastal Union ambao walishawahi kutwaa ubingwa wa Bara, walimaliza wa mwisho kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 22, huku mahasimu wao African Sports wakimaliza nafasi ya 15 baada ya kujikusanyia pointi 26 na Mgambo JKT wakimaliza nafasi ya 14 na pointi 28.

Kufuatia timu zote za Tanga kushushwa daraja, ni dhahiri hakutakuwa na mechi yoyote ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani msimu wa 2016/17.

*Yanga yatinga makundi

Mabao mawili kipindi cha pili yaliyofungwa na Simon Msuva na Anthony Matheo, yaliipa Yanga ushindi dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola katika mchezo wa kwanza kupata timu itakayotinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo wa marudiano uliochezwa mjini Dundo, Angola ulishuhudia wenyeji Sagrada Esperanca wakichomoza na ushindi wa bao 1-0 ambalo hata hivyo halikutosha kuzima ndoto za Yanga kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

*Yanga yabeba taji jingine

Wiki chache tu baada ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga iliifunga Azam FC 3-1 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kutwaa Kombe la FA.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Amissi Tambwe aliyetupia kambani mabao mawili na Deus Kaseke huku lile la kufutia machozi na Azam FC likifungwa na Didier Kavumbagu.

Bingwa wa Kombe la FA anaiwakilisha Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kwa sababu Yanga tayari ni bingwa wa Ligi Kuu Bara na kujihakikishia kucheza Klabu Bingwa Afrika, nafasi hiyo inakwenda kwa Azam FC.

*Azam Media yamwaga fedha

Kampuni ya Azam Media imeingia mkataba wa kiasi cha shilingi bilioni mbili na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kudhamini ligi ya wanawake na ile ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema wameamua kumwaga fedha kwa mashindano hayo mawili kwa nia ya kuendeleza mchezo wa soka.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alisema moja ya masharti ya mkataba huo ni kila timu ya Ligi Kuu Bara kuwa na kikosi kizuri cha vijana chini ya umri wa miaka 20 na timu yoyote itakayoshindwa kutimiza masharti hayo itashushwa daraja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -