Monday, November 30, 2020

YANGA YAVUNA ILICHOPANDA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga, imevuna ilichopanda kwa wiki nzima kwenye mazoezi yao baada ya jana kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 37, wakiendelea kubaki nafasi ya pili nyuma ya vinara Simba, wenye pointi 38 kabla ya mchezo wao wa leo dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja huo.

Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Ludovic Charles kutoka Tabora, Yanga ilijikuta ikishangazwa na wapinzani wao hao baada ya nyavu zao kutikiswa dakika ya 59 na Ludovic Venance, aliyemalizia vema pasi murua kutoka kwa kiungo wa zamani wa Wana-Jangwani hao, Abdallah Mguhi, ikiwa ni baada ya mabeki wake kuzembea katika kukaba.

Matokeo hayo yameifanya Lyon kufikisha pointi 19, lakini ikibaki katika nafasi iliyokuwapo ya 12, baada ya kushuka dimbani mara 17, sawa na Yanga.

Licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, Yanga walijikuta wakiambulia bao moja tu lililofungwa kwa kichwa na Amissi Tambwe, kutokana na krosi ya Juma Abdul dakika ya 76.

Matokeo hayo ya Yanga yanakuja ikiwa ni baada ya madai ya kuwapo kwa mgomo wa wachezaji, wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya Novemba na hivyo kudaiwa kugomea mazoezi.

Japo uongozi wa Yanga umekuwa ukikanusha hilo la mgomo, lakini imedaiwa kuwa, wachezaji wa timu hiyo walikuwa wakifika mazoezini, lakini wakikataa kufanya lolote zaidi ya kupiga stori na kuondoka kuendelea na hamsini zao.

Katika kuthibitisha ukweli wa jambo hilo, baada ya mchezo wa jana, mashabiki wa Yanga walionekana kupandwa na hasira na kutaka kuwashambulia wachezaji wao, lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na ulinzi mkali uliowekwa na askari waliokuwa uwanjani hapo.

Ukiachana na hilo, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, jana alifanya mabadiliko yaliyowaacha mdomo wazi mashabiki, akikumbushia enzi za kocha marehemu Syllerysaid  Mziray.

Baada ya kuona mambo ni magumu, Mzambia huyo aliwaingiza washambuliaji wake watatu, Obrey Chirwa, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya, kuchukua nafasi za Thaban Kamusoko, Deus Kaseke na Mwiji Haji.

Kati ya nafasi hizo, kitendo cha kumtoa beki wa kushoto, Haji na kumwingiza winga Mwashiuya ili kumtumia kama wingi beki, kilikumbushia enzi za Mziray alipokuwa akimtumia Kenneth Mkapa kama wingi beki, akipanda kusaidia mashambulizi na kurudi kukaba, pale mambo yalipoelekea kwenda kombo.

Kwa ujumla mchezo wa jana ulikuwa na ushindani wa aina yake, kwani Lyon walionekana kupania vilivyo kupata ushindi.

Dakika tano kabla ya mchezo kumalizika, Yanga nusura wapate bao la ushindi kupitia kwa Martin, baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Lyon, lakini uimara wa safu ya ulinzi ‘wabishi’ hao iliyokuwa chini ya nyota wa zamani wa Simba, Miraji Adam na Hassan Isihaka, uliwafanya Wana-Jangwani hao kuambulia patupu.

Katika mchezo huo Yanga walikosa huduma ya mshambuliaji wao, Donald Ngoma, aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kikosi cha Yanga kilikuwa:  Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji/Geoffrey Mwashiuya (dk77), Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Said Makapu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko/Obrey Chirwa (dk75), Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke/Emmanuel Martin (dk 65).

African Lyon: Rostand Youthe, Miraji Adam, Halfan Twenye, Hamadi  Waziri, Hamad  Manzi, Hassan Isihaka, Omary Abdallah/Peter Mwalyanzi (dk81), Awadh  Juma/Ludovic Venance (dk46), Thomas Mourice/Cosmas Lewis (dk82) na Abdalah  Mguhi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -