Sunday, October 25, 2020

YANGA YAZALIWA UPYA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA

.Ni baada ya ziara ya Zenji

.Wavuna vifaa vipya viwili, Fei Toto chamtoto

KIKOSI cha Yanga kilichokuwa Zanzibar, kimerejea jijini Dar es Salaam huku kikiwa kimezaliwa upya tayari kuendelea kuuwasha moto Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na nondo walizozipata visiwani humo.

Yanga ilikimbilia Zanzibar kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wakongwe wa soka wa visiwani humo, Malindi, lakini pia Wanajangwani hao wakifuata baraka kutoka kwa wanachama na mashabiki wao wa huko wakiwamo ‘wazee’ wao.

Na baada ya kutua Dar es Salaam, mabosi wa Yanga wameonekana kuwa na furaha tele, wakitamba kikosi chao kimezaliwa upya na hivyo watapambana kadiri ya uwezo wao kuhakikisha hawafanyi makosa yatakayowazuia kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kama msimu uliopita walipowapa mwanya watani wao wa jadi, Simba, kubeba ‘mwali’ wa kipute hicho.

Yanga ni miongoni mwa timu nne ambazo hazijapoteza mechi ya ligi mpaka sasa, zaidi ya kutoka sare dhidi ya Simba katika mechi zake sita ilizocheza, huku watani wao hao wakiwa wamefungwa moja na kupata sare mbili.

Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh, alisema ziara yao ya Zanzibar ilikuwa nzuri, hasa baada ya kukutana na wadau mbalimbali ambao wameipandisha mzuka timu hiyo kuelekea harakati zao za mbio za ubingwa.

“Ziara ilikuwa nzuri, tunashukuru tumerejea salama na tumefaidika nayo baada kukutana na wanachama na mashabiki ambao wana lengo la kuona timu hii inafanya vema zaidi.

“Wanachama hao wengi wanataka kuona timu hii msimu huu inachukua ubingwa wa Ligi Kuu na ikiwezekana mapema, ila siwezi kuwataja majina. Kwa kweli kila mtu ndani ya timu kwa sasa ana ari na nguvu mpya ya kuipigania timu katika mechi zetu za Ligi Kuu na mashindano mengineyo tutakayoshiriki,” alisema Saleh.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema baada ya kumaliza mchezo wao na Malindi walioshinda mabao 2-0, kwa sasa wanaangalia mchezo ujao, lengo lao likiwa ni ushindi ili kujiweka pazuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.

“Ligi ni ngumu kutokana na ushindani uliopo, ila baada ya kutoka Zanzibar, tutakuwa na programu maalum ili kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa,” alisema.

Akizungumzia mchezo wao ujao dhidi ya Alliance ya Mwanza, Mwandila alisema kikosi hicho leo kitaendelea na mazoezi kama kawaida kujipanga vilivyo kuwasambaratisha wapinzani wao hao.

Yanga inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, baada ya kujikusanyia pointi 16 kutokana na mechi sita, ikiwa nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 17 na mechi tisa, huku vinara wakiwa ni Azam waliovuna pointi 18 kwa mechi nane.

Baada ya kutamba katika ligi hiyo kwa misimu minne waliyotwaa ubingwa kati ya mitano, msimu uliopita Yanga waliporwa taji na Simba, hivyo msimu huu wakongwe hao wametamba kurejesha ufalme wao Jangwani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -