Sunday, January 17, 2021

Yanga yazidi kukiimarisha kikosi chao

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA,

UTAMU wa kikosi cha Yanga sasa unazidi kukolea, baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuendelea kuimarisha safu ya benchi la ufundi na pia kukiimarisha kikosi chao.

Jana aliyekuwa msaidizi wa kocha George Lwandamina kwenye kikosi cha Zesco, Noel Mwandila, ametua nchini kwa lengo la kukaa benchi moja na Lwandamina ili kuinoa timu hiyo.

Mwandila amekuja Yanga ikiwa ni kutokana na mapendekezo ya Lwandamina aliyesaini mkataba wa kuinoa timu hiyo mwezi uliopita akitokea Zesco ya Zambia.

Mwandila ambaye ni kiungo wa zamani wa timu ya Green Buffalos ya Zambia, anatarajiwa kuanza majukumu yake muda wowote kuanzia sasa, baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga.

Enzi zake akiwa kama mchezaji, Mwandila alikuwa ni mmoja wa viungo hodari wa timu mbalimbali alizozichezea katika nchi za Zambia, Afrika Kusini na Malaysia.

Mwandila ambaye licha ya kuwa kiungo fundi na kuaminika enzi hizo, ameweza kujizolea umaarufu mkubwa jijini Lusaka kutokana na kufanya vema kwenye ligi ya nchi hiyo pamoja na kutwaa makombe mbalimbali.

Mbali na ujio wa kocha huyo, tayari Justine Zulu amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo wakati Winston Kalengo ambaye ni mshambuliaji, anatarajiwa kutua siku yoyote kuanzia sasa.

Kama Yanga itafanikiwa kumleta Kalengo ambaye ni mfungaji mwenye rekodi za kutisha za Zesco, basi itakuwa na kikosi cha kutisha msimu huu wa michuano ya kimataifa hasa kutokana na mabadiliko waliyoyafanya.

Yanga sasa itakuwa na makocha wanne, ambapo ni pamoja na Mwandila, Juma Mwambusi, Juma Pondamali na Lwandamina chini ya Hans Van Pluijm.

Katika hatua nyingine, kocha Lwandamina amemuibua mshambuliaji wa timu hiyo, Malimi Busungu ambaye baada ya kupewa darasa zito na kocha huyo, ameapa kurejea katika ubora wake  maradufu.

Busungu ambaye aliwekwa kitimoto juzi na Pluijm na Lwandamina, alipewa maneno mazito yaliyomtaka kubadili mwenendo wa maisha yake kama anataka kucheza mpira.

“Naweza kusema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nimejipanga kuisaidia timu yangu ndio maana nimerudi kwa kasi na ari mpya, kila kitu kinawezekana tusahau yaliyopita sasa tufanya kazi,” alisema Busungu.

Mshambuliaji huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia, lakini hata alipopona alishindwa kurejea katika kiwango chake na hivyo kujikuta akipoteza namba kwenye kikosi cha Yanga.

Katika hatua nyingine, Vigogo wa Yanga jana walivamia kwenye mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Viongozi waliokwenda kushuhudia mazoezi hayo ni makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga, Katibu wa Kamati ya Mashindano, SamwelLukumay, Isaack Chanji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na kocha msaidizi, Noel Mwandila aliyetua nchini jana akitokea Zambia.

Katika mazoezi hayo, winga wa timu hiyo, ObreyChirwa alikiona cha moto baada ya kupewa programu ya kufanya mazoezi kuzunguka uwanja mzima wakati wenzake wakiendelea na mazoezi ya pamoja.

Chirwa alipewa adhabu ya kuzunguka uwanja kwa sababu ya kuchelewa kujiunga na wenzake katika mazoezi yaliyoanza Jumatatu wiki hii kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini  jijini Dar es Salaam.

Winga huyo alirejea jana usiku wa manane akitokea nchini kwao Zambia ambako alikwenda kumpumzika, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Katika mazoezi hayo, Lwandamina alionekana kuanza na kiungo, Said Juma Makapu ambaye kwa muda mwingi alikuwa akimpa mbinu mbalimbali za kucheza, huku akimchezesha katika kikosi chake cha kwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -