Sunday, November 29, 2020

YANGA, ZIMAMOTO, KVZ SAFARI NDIO IMEANZA MSIBWETEKE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

YANGA na wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya kimataifa wameanza vizuri baada ya kupata matokeo ya ushindi nyumbani na ugenini.

Wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, upande wa Tanzania Bara, Yanga yenyewe ilipata ushindi wa mabao 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro dhidi ya wenyeji Comoro.

Nao Zimamoto ambao walikuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa kupambana na Ferroviario de Beira ya Msumbiji, walipata ushindi wa mabao 2-1 mechi iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Wawakilishi wengine timu ya KVZ nao waliwafunga Le Messager Ngozi ya nchini Burundi kwa mabao 2-1 mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Timu zetu zote zimejiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwani itahitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mechi za marudiano zitakazofanyika wikiendi hii.

Wawakilishi hao wote wanahitaji kupata sare ya aina yoyote ugenini ili kutinga raundi ya kwanza kitu ambacho huenda kisiwe rahisi kwao kama hawatajipanga vema.

Inawezekana kazi ikawa rahisi kwa Yanga kuliko Zimamoto na KVZ zitakazocheza ugenini, kwani wenyeji wao watakuwa wakihitaji ushindi usiopungua bao 1-0 ili kuzitupa nje timu zetu ila soka ni mchezo usiotabirika.

Kama wapinzani hao walifungwa katika mechi ya awali si ajabu kwa timu za Tanzania nazo kufungwa kama hazikuwa makini kwa sababu soka ni mchezo wa makosa na kila timu moja inapokosea ndivyo inavyoadhibiwa.

Kitu muhimu ni wachezaji wa timu zote na makocha wao kurekebisha dosari ambazo zilitoa mwanya kwa wapinzani hao kupata mabao.

Timu zetu zore ziliruhusu nyavu zao kuguswa Yanga ilishinda 5-1, KVZ na Zimamoto zilishinda kila mmoja mabao 2-1, lazima kuna tatizo kati safu zao za ulinzi.

Tunategemea timu zetu zitafanya vizuri endapo tu zitajituma na kutambua kwamba wao ni wawakilishi wa Watanzania zaidi ya milioni 40.

Wawakilishi hao wanapaswa kutambua kwamba, Watanzania wanahitaji ushindi na si vinginevyo wapambane kikamilifu ili kuhakikisha zinasonga mbele kwenye hatua inayofuata.

BINGWA tunatoa angalizo au ushauri kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo, kazi ndio imeanza wanatakiwa kuacha kasumba za timu zetu za hapa Tanzania kubweteka pale wanapoona wamepata mafanikio kidogo.

Kama safari basi ndio imeanza sasa, kikubwa uongozi na benchi la ufundi liendelee na mipango ya kuhakikisha timu zinafanya vizuri kwenye hatua inayofuata.

Najua Yanga wamewadharau Ngaya ila hawapaswi kuichukulia poa badala yake irudiane nao kana kwamba wanacheza mechi ya fainali.

Muda huu ni wa kusaka mbinu na mipango ya kuzimaliza timu hizo pinzani kwenye mchezo wa marudiano wikiendi hii.

Nina amini kwamba ushindi huo si mkubwa, unaweza kupinduliwa kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia katika mechi mbalimbali hasa kama na wao hawatakuwa makini katika mchezo huo wa marudiano.

Uwezo wa timu hizo pinzani kupata mabao kama ambavyo Yanga na wawakilishi wengine wamefanya nyumbani upo, hivyo basi ni muhimu sana kujipanga vyema kuhakikisha inapata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kupata bao la mapema.

Ni matumaini yetu kwamba benchi la ufundi la Yanga na Zimamoto sambamba na KVZ, limeona makosa yaliyojitokeza kwenye michezo ya kwanza hasa katika safu ya ushambuliaji ambayo ingeweza kupata mabao mengi zaidi, kwamba watayafanyia kazi na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mechi ya marudiano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -