Thursday, November 26, 2020

Yondani aliza mashabiki Moshi

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TIMA SIKILO NA MWAMVITA MTANDA, MOSHI

YANGA jana imechapwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Uhsirika mjini hapa, huku beki wa kati wa Wanajangwani hao, Kelvin Yondani, akiwatoa machozi mashabiki.

Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya Yanga kuelekea mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers itakayopigwa ugenini wiki ijayo.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo Wanajangwani hao kuwa na shughuli pevu kupata ushindi au sare ya zaidi ya mabao 2-2 ugenini ili kusonga mbele.

Akifahamu kibarua hicho kilichopo mbele yao, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kukichimbia kikosi chake mjini hapa, huku wakipanga kucheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Polisi Tanzania jana na kesho wakiivaa AFC Leopard ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Katika mchezo huo wa jana, kikosi cha Yanga hakikuonyesha kandanda la kuvutia, hali iliyowapa mwanya wapinzani wao kutamba na kupata ushindi huo, bao la kwanza likifungwa na Marcel Kaheza kwa mkwaju wa penalti dakika ya tano, baada ya Ally Ally kuunawa mpira eneo la hatari.

Bao la likiwekwa kimiani na Ditram Nchimbi katika dakika ya 74 na kuzima kabisa matumaini ya mashabiki wa Yanga mjini hapa na maeneo ya jirani kuiona timu yao ikitoka uwanjani na ushindi.

Walikuwa ni Polisi Tanzania waliokuwa wa kwanza kulisakama lango la Yanga ambapo dakika ya 14, walifanya shambulizi la nguvu lililoishia kuwa kona tasa.

Yanga walijibu mapigo dakika ya 18 lakini Simon Gustafu alishindwa kulenga lango baada ya kutokea piga nikupige katika goli la Polisi Tanzania.

Mshambuliaji mpya wa Yanga, David Molinga, nusura aipatie timu yake hiyo bao dakika ya 80, lakini shuti lake la mpira wa adhabu alilopiga kwa ufundi, liliokolewa na kipa wa Polisi, Mohammed Yusuph.

Katika mchezo huo, Zahera hakuwatumia wachezaji wake nyota wakiwamo Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Mohammed Issa ‘Mo Banka’, Muharami Issa ‘Marcelo’, Juma Balinya na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Zahera aliwalaumu baadhi ya wachezaji aliowapanga kwa kutoonyesha kiwango, zaidi wakiwa ni wapya Kalengo, Ally na Bigirimana.

“Kikosi nilichokipanga nimejaribu kuwapa nafasi wachezaji wengine kuona kile wanachokifanya, lakini nimeona wengine bado wanacheza vibaya…sasa kama wanaendelea hivi, tusije kulaumiana,” alisema.

Katika hatua nyingine, mashabiki wa Yanga walijikuta wakitokwa na machozi wakimlilia Yondani wakidai kuwa beki huyo ni muhimu mno ndani ya kikosi chao.

Tukio hilo lilitokea kabla ya mchezo huo wa jana ambapo baadhi ya mashabiki waliokuwa wamejazana mlangoni, walisikika wakisema wamefika uwanjani hapo ili kumwona Yondani tu.

Akizungumza na BINGWA kwa niaba ya wenzake, shabiki wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Ally Mrombo, alisema wamefarijika mno Yondan kurejea kikosini.

Alisema baada ya kuona uwezo wa Lamine Moro, wanaamini akicheza pamoja na Yondani, hakuna mshambuliaji wa timu pinzani anatakayeweza kuipenya safu yao ya ulinzi kirahisi.

“Tumekuja kuona kikosi chetu, tumefurahi kumuona ‘baba mwenye nyumba’ Kelvin Yondani amerejea kikosini, tunampenda sana. Akicheza pamoja na Lamine, watakoma.

“Pia, hawa wachezaji wetu wapya, Patrick Sibomana na wenzake, wapo vizuri. Tunaushukuru uongozi kwa kutuletea wachezaji wetu tuwaone ‘live’,” alisema Mrombo.

Katika mchezo huo wa jana, kikosi cha Yanga kilikuwa hivi; Ramadhani Kabwili/Farouk Shikalo, Moustafa Selemani/Juma Abdul, Gustafa Simon/Jaffari Mohammed, Ally Ally, Kelvin Yondani/Said Juma Makapu, Abdulaziz Makame, Maybin Kalengo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, David Molinga, Rafael Daudi na Deus Kaseke/ Issa Bigirimana.

Polisi Tanzania: Mohammed Yusuph, William Lucian ‘Gallas’/Shabani Stambuli, Yassin Mustafa, Othman Mmanga, Iddi Mobi, Baraka Majogoro, Andrew Chamungu/Pato Ngonyani, Nassor Abbal, Ditram Nchimbi, Marcel Kaheza/ Erick Msagati na Sixtus Issabilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -