Friday, October 30, 2020

YONDANI ‘OUT’, NINJA APETA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


NAHODHA na beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani, ataukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United, baada ya kuoneshwa kadi tatu za njano katika mechi za ligi hiyo, hivyo kutoa nafasi kwa Shaibu Abdallah ‘Ninja’, kuchukua nafasi yake.

Yondani amejikuta akiigharimu Yanga kwa wakati huu ambao timu yake hiyo imeonekana kuwa na kasi ya aina yake kwa kushinda mechi zao zote tatu za ligi hiyo inayohusisha timu 20.

Beki huyo juzi alionyeshwa kadi ya njano ya tatu wakati Yanga ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao hilo pekee la ushindi, lilifungwa na mshambuliaji tegemeo wa Yanga, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Makambo, baada ya kuitokea kiufundi pasi ndefu ya Ibrahim Ajib.

Kutokana na kukosekana kwa Yondani, safu ya ulinzi ya kati inatarajiwa kuundwa na Vincent Andrew ‘Dante’ akisaidiana na kati ya Ninja, Pato Ngongani au Said Juma Makapu, kutegemea na mapendekezo ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, raia wa DRC.

Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, alikiri kikosi chao kumkosa Yondani dhidi ya Singida United baada ya kufikisha kadi tatu za njano.

“Ni kweli Yondani amefikisha kadi tatu za njano, hivyo hataweza kucheza mchezo wa Jumapili dhidi ya Singida United,” alisema Hafidh.

Yanga hadi sasa imeshinda mechi za ligi hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar mabao 2-1, Stand United mabao 4-3 na ushindi wa bao 1-0 walipovaana na Coastal Union juzi, hivyo kujikusanyia pointi tisa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -