Wednesday, October 21, 2020

YONDANI: YANGA MSITISHIWE NYAU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA

BEKI tegemeo wa Yanga, Kelvin Yondani, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutoumizwa kichwa na kitendo cha Simba kuwa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara kwani wanawajulia vilivyo watani wao hao wa jadi linapokuja suala la kupigania ubingwa.

Yondani ambaye ameufanya ukuta wa Yanga kusimama imara hadi sasa, akishirikiana na Vincent Bossou, aliyasema hayo juzi alipokuwa kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili.

Akizungumzia mbio za ubingwa wa Bara, Yondani alisema kuwa hakuna timu inayoweza kuwapora taji hilo japo Simba wapo kileleni kwa sasa kwa tofauti ya pointi mbili.

“Simba watasubiri sana kwa kweli, waendelee kuongea tu, sisi tunafanya yetu na lazima taji la VPL liwe ndani ya Mtaa wa Jangwani, pale Kariakoo… ingekuwa ni Azam ndio wapo mbele yetu, angalau tungekuwa na hofu, lakini si Simba,” alisema.

Yondani mwenye umbo la kawaida, lakini akiwa ni hodari wa kucheza mipira ya juu kwa kichwa, alisema kinachompa jeuri kuiondoa Simba kwenye mbio za ubingwa ni uzoefu wao katika ligi pamoja na jinsi wanavyofahamu kucheza na akili za watani wao hao.

Alisema kwenye kikosi chao, wanajivunia uwepo wa wachezaji wengi wenye uwezo wa kufanya lolote ndani ya dakika yoyote ile.

Yondani ambaye anatumia akili na nguvu kwenye kukaba, akiwa ni kizingiti kwa mastraika wakorofi, alisema hata kama Simba watashinda mechi zao zote, watakapokutana nao lazima watawapiga na hivyo kulitetea taji lao.

Yondani alimzungumzia straika wa zamani wa Simba ambaye pia aliwahi kukipiga Jangwani, Emmanuel Okwi, aliyetemwa na klabu ya Sonderjyske ya Denmark, kwamba hata kama atarejea Msimbazi, hilo haliwaumizi kichwa hata kidogo.

“Okwi tunamjua sana na tulishacheza naye, pia sidhani kama atakuwa na mpya kiivyo kama wanavyofikiria, hivyo wamlete tu atatukuta,” alisema.

Yondani alimmwagia sifa kocha mkuu wao, Geogre Lwandamina, kwamba ni mwenye uwezo wa hali ya juu wakiamini ataifikisha timu yao kwenye mafanikio makubwa msimu huu.

“Tunaendelea na mazoezi kama kawaida na tuna kocha anayejua vema wachezaji, hivyo Mwadui wajiandae, sisi tupo kamili kwa mchezo wa Jumapili (kesho),” alisema.

Yanga inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kuvaana na Mwadui, mchezo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -