Sunday, January 17, 2021

YOTE KHERI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

>>Mambo matano muhimu yaliyojitokeza Arsenal vs B’mouth

>>Edie Howe alimnyanyasa Arsene Wenger na Arsenal yake

>>Je, Arsenal wamepoteza matumaini ya ubingwa?

LONDON, England

MATUMAINI ya ubingwa wa Ligi Kuu England kwa klabu ya Arsenal msimu huu yanaanza kufifia baada ya kupata matokeo ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia jana kwenye dimba la Vitality.

Hayakuwa matokeo mazuri kwa upande wao kwani iliwabidi kusubiri hadi dakika 20 za mwisho kurudisha mabao matatu waliyofungwa ndani ya dakika 50 za kwanza.

Bournemouth walikuwa wa kwanza kuliona lango la Arsenal kwa mabao ya Charlie Daniels, Callum Wilson na Ryan Fraser kabla ya vijana wa kocha Arsene Wenger kurudi kwa kasi na kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Alexis Sanchez, Lucas Perez kabla ya Olivier Giroud kufunga bao la tatu na kuiokoa timu yake isiaibike na kichapo hicho cha aibu.

Kutokana na matokeo hayo, Arsenal ilisalia katika nafasi ya nne na pointi zao 41, ikiachwa nyuma na vinara wa ligi, Chelsea kwa tofauti ya pointi nane. Chelsea walitarajiwa kukabiliana na Tottenham Hotspurs usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa ligi hiyo.

Haya hapa ndiyo mambo matano muhimu yaliyojitokeza kwenye mtanange huo wa juzi usiku.

Arsenal inazidi kuachwa mbio za ubingwa

Ingawa walisawazisha mabao yote matatu, kitendo cha kutoka sare ugenini huku ukiruhusu nyavu zako kutikiswa mara tatu na timu iliyopo nafasi sita chini yako kinamaanisha kwamba hauna ubavu wa kushindania taji la ligi.

Arsenal walitakiwa kufanya jitihada za dhati kushinda mchezo huo ili waendelee kuwapa presha vinara wa ligi, Chelsea lakini walishindwa kufanya hivyo. Je, watapunguza lini ‘gepu’ la pointi nane lililopo baina yao? Swali gumu katika wakati mgumu.

Inategemea na matokeo ya usiku wa kuamkia leo, lakini kwa jinsi Chelsea ilivyo na kasi hakuna uhakika wa vijana hao wa Antonio Conte watapoteza pointi nyingi hadi kufikia Mei mwaka huu.

Hali ngumu wanayopitia kwa sasa pia inatokana na ‘ujeuri’ wao wa kutosajili mchezaji wa kiwango cha dunia katika sehemu walizotakiwa kufanya hivyo.

Ukweli ni kwamba, Bournemouth wanatakiwa kupewa pongezi kwa kiwango cha hali ya juu walichokionesha kwenye mchezo huo lakini kwa mara nyingine vijana wa Wenger walisikitisha.

Mwaka mpya Arsenal ile ile

Bao la kwanza la Bournemouth lililofungwa na Daniels lilitokana na nafasi kubwa aliyoachiwa na wachezaji wa Arsenal waliotakiwa kumkaba, Hector Bellerin na Aaron Ramsey.

Daniels alijikuta akipokea pasi ndefu ya juu huku akiwa hana mtu wa kumzuia, akaituliza bila presha na kumfunga Petr Cech bila wasiwasi.

Kama safu ya ulinzi ya Arsenal itaendelea kufanya uzembe wa namna hiyo, hawatapoteza matumaini ya ubingwa pekee bali wataondoshwa hata kwenye zile nafasi nne za juu.

Bournemouth imeimarika mno

Matokeo ya sare yameisaidia ‘Cherries’ kubakia kwenye nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu England na hata kama hawapati matokeo mazuri kila mara bado wanaonesha uwezo wa kung’ang’ania katika 10 bora msimu huu.

Klabu hiyo iliweza kujikwamua katika janga la kushuka daraja kutokana na pointi tisa walizozikusanya kwenye ushindi wa mechi zao tatu za Desemba mwaka jana dhidi ya Liverpool, Leicester na Swansea.

Hivi karibuni watakabiliana na Milwall katika mchezo wa kuwania Kombe la FA huku michezo yao ya ligi itakayofuata mwezi huu ikiwa ni dhidi ya Hull City, Watford na Crystal Palace. Hawana budi kushinda michezo hiyo.

Xhaka ataigharimu Arsenal

Kiungo Granit Xhaka, alinyakuliwa na Arsenal kutoka Borussia Monchegladbach kwa ada ya pauni milioni 35 kwa lengo la kuiongezea nguvu safu ya kiungo hasa kwenye eneo la ulinzi.

Na licha ya kuonesha uwezo wa hali ya juu, Xhaka ameshaonesha upande wa pili wa soka lake dimbani. Ni mtata kwenye maeneo yanayohitaji utulivu.

Dhidi ya Swansea Oktoba mwaka jana, alioneshwa kadi nyekundu na ni kawaida yake kucheza soka la nguvu pale mchezo unapobadilika.

Arsenal kwa sasa haihitaji kuwakosa wachezaji muhimu na Xhaka hana budi kucheza kwa utulivu kwenye kipindi hiki kigumu cha ligi hasa baada ya kiungo mkabaji wao, Francis Coquelin, kuanza kusumbuliwa majeruhi.

Howe alimnyanyasa Wenger

Mwaka jana, kocha wa Bournemouth, Edie Howe, alizungumziwa kuwa huenda akapewa kibarua cha kuinoa Arsenal.

Kikosi cha kocha huyo kinajulikana kwa soka safi wanalocheza bila kujali wanapambana na timu ya aina gani, hawana desturi ya kupaki basi kama zilivyo timu nyingine ndogo za ligi hiyo.

Howe alionesha ufundi wa mifumo dhidi ya Wenger kwa takribani dakika 60 za mchezo huo.

Kikosi chake kilisukuma mashambulizi ya nguvu na kuilazimisha Arsenal ifanye makosa lukuki kutokana na presha waliyokuwa wakipatiwa na vijana hao wadogo na wenye kasi.

Kwenye ulinzi pia, Bournemouth walikaba kwa nidhamu na ushirikiano kiasi cha kuwafanya Arsenal wahangaike kupiga shuti la kulenga goli kwa dakika 70 za mchezo huo.

Kiufupi, Wenger alikuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwa Howe.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -